Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkwasa amkataa Zahera mapema tu Yanga

Muktasari:

Mkwasa tangu akabidhiwe Yanga baada ya Zahera kufurushwa Jangwani, timu yake imeshinda mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Bara ikiwamo ile ya 1-0 dhidi ya Ndanda na ya juzi kuwafumua JKT kwa mabao 3-2 na mashabiki wakipigia chapuo akabidhiwe timu jumla kwa kubadilika kwa kikosi.

Dar es Salaam. Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa amezidi kuwapa mzuka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo baada ya Ijumaa kupata ushindi dhidi ya JKT Tanzania, lakini kocha huyo amefunguka akitaka asifananishwe kabisa na mtangulizi wake, Mwinyi Zahera.
Mkwasa tangu akabidhiwe Yanga baada ya Zahera kufurushwa Jangwani, timu yake imeshinda mechi mbili mfululizo za Ligi Kuu Bara ikiwamo ile ya 1-0 dhidi ya Ndanda na ya juzi kuwafumua JKT kwa mabao 3-2 na mashabiki wakipigia chapuo akabidhiwe timu jumla kwa kubadilika kwa kikosi.
Kocha huyo, alifichua mabadiliko hayo yamekuja kupitia mazoezi ambayo anawapa wachezaji wake na kutaka asilinganishwe kwa kila anachokifanya kwa kutazamwa na yale ya Zahera.
“Kila mtu anaona kabisa namna tunavyocheza, huko nyuma mnajua walivyokuwa wanacheza na watu wanasema hivyo bado najaribu kuweka timu iwe sawa na muunganiko mzuri,” alisema.
Mkwasa aliongeza kwa kusema licha ya kwamba wanapata matokeo, bado anaendelea kukisuka kikosi hiko ili kiweze kuwa bora zaidi msimu huu.
“Bado najenga timu mpaka hivi sasa, kwa mfano ukiangalia Makame alikuwa yupo Taifa Stars na alirejea tukiwa tuna muda mchache kuja katika mechi hii, nilimpa muda wa kupumzika na kunyoosha misuli, sikumpanga kwani hakuwepo na hajui tulikuwa tunafanya nini ndio maana akaingia kipindi cha pili,” alisema.