Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mkongo wa Yanga awasapraizi Wagosi

Muktasari:

  • Mwanaspoti lilipomuuliza amekuwa akitoa mara kwa mara kwa wenye mahitaji maalumu, msukumo huo unatokana na nini! Alijibu anapokuwa nacho anaamini wengine hawana.

HUYU Mwinyi Zahera achaneni naye kabisa, kwani unaambiwa kitu alichofanya Mkwakwani kimewashangaza wakazi wa jijini Tanga. Ipo hivi. Mara baada ya kumalizika kwa pambano lao dhidi ya Coastal Union, kocha huyo kutoka DR Congo aliwafanya sapraizi walemavu wa miguu watembeleao baiskeli maalumu.

Zahera aliwaona walemavu hao wakiwa wameketi pembeni mwa uwanja baada ya kumaliza mahojiano yake na Wanahabari alimtuma shabiki mmoja awaite. Watu wenye ulemavu wapatao watano walipokutana na Zahera alitoa Sh 100,000 kisha akawaambia hana kikubwa kaamua kugawana nao.

“Nawapenda sana na Mungu awabariki, niliwaona wengi ili mradi mmerudi wachache chukueni hiki hapa,” anafungua pochi yake na kuwapa pesa.

Mwanaspoti lilipomuuliza amekuwa akitoa mara kwa mara kwa wenye mahitaji maalumu, msukumo huo unatokana na nini! Alijibu anapokuwa nacho anaamini wengine hawana.

“Napenda kutoa sadaka kwa njia mbalimbali sijali ni mashabiki wa Yanga ama Simba kwangu ubinadamu ni jambo kubwa ni kitu kinachotoka ndani ya moyo wangu” alisema. Achilia mbali sadaka aliyoifanya kwa walemavu hao, pia kuna jambo aliloliona kwenye Ligi Kuu Bara linalofanya soka lidumae kwamba ni Usimba na Uyanga.