Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Miraji Athuman atamani kikosi cha kwanza Simba

Muktasari:

Simba imesajili kikosi cha ushindani, jambo hilo linamfanya winga wa timu hiyo, Miraji Athuman kuwa na kazi maalumu ya kuhakikisha kocha Patrick Aussems anamuelewa

WINGA mpya wa Simba, Miraji Athuman amesema anachokipigania kwa sasa ni kuhakikisha kocha mkuu Patrick Aussems anamshawishi ili kupangwa kikosi cha kwanza.
Aussems amekuwa akimpa nafasi mchezaji huyo na mechi yao ya ufunguzi alifunga bao moja, Simba ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKT Tanzania.
Mchezaji huyo amesema anatamani kufanya kazi na sio kuwa mchezaji wa kusugua benchi, akidai anaamini nidhamu na juhudi ndivyo vitakavyofanya afikie anachokiwaza.
"Huwa najipa moyo kwamba ninaweza licha ya Simba kuwa na wachezaji wazoefu ambao uwezo wao upo wazi, hilo haliwezi kuninyima raha kwamba nitakuwa sipati namba"

"Mchezaji ambaye ananifanya nijiamini nitaweza kuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi cha kwanza ni Shiza Kichuya alitoka Mtibwa Sugar na akafanya maajabu, hata mimi nitafanya maajabu,"anasema.