Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mgunda: Wagosi Mtuombee

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Juma Mgunda amesema kuwa anawaomba wadau na wapenzi wa Soka kuiombea timu hiyo ili iepuke kutoshuka daraja baada ya kuwa na matokeo ya kutoridhisha msimu huu licha ya timu hiyo kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui kwenye mchezo uliopita.

Mgunda amesema kuwa licha ya ushindi kwenye mechi iliyopita ila bado wana kazi kubwa ya kufanya kwenye mchezo wao wa leo watakapokuwa katika uwanja wao wa nyumbani Mkwakwani Tanga kukabiliana na 'Wanankurukumbi' Kagera Sugar kuhitimisha msimu huu.

"Ushindi kwenye mechi yetu iliyopita umeongeza ari kwa wachezaji wangu kuelekea mechi yetu ya leo na Kagera Sugar lakini nichukue nafasi hii kuwaomba wadau wa Mpira watuombee ili tufanye vizuri katika mchezo wetu wa mwisho ili Coastal Union waendelee kuiona Ligi Kuu kwa msimu ujao" amesema

Katika mchezo dhidi ya Mwadui Fc mashabiki wa timu hiyo walikuwa na mabango yaliyokuwa yakihitaji kocha huyo kuachia timu hiyo hata kama itasalia Ligi Kuu msimu ujao kutokana na kutokuwa na imani na kocha huyo baada ya kuwa na matokeo mabaya ya kutoridhisha hali iliyomfanya Mgunda kusema kuwa sio wakati  sahihi wa kulizungumzia hilo bali anachoangalia ni kuipigania timu hiyo isishuke daraja.

"Naheshimu mawazo ya mashabiki kwa kuwa wao siku zote wanahitaji furaha ila niwaombe tu kuwa kwa sasa sio wakati sahihi kwa mashabiki kufikia hatua hiyo ambayo bado timu iko kwenye wakati mgumu na inawahitaji kwa ajili ya kuipa sapoti katika mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar" amesema

Coastal Union inapambana kuepuka kushuka daraja kwani haiko kwenye nafasi nzuri kwenye msimamo wa Ligi Kuu ikiwa katika nafasi ya 14 ikiwa na pointi 37 huku Kagera Sugar ikiwa nafasi ya 11 ikiwa na pointi 40.


IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI