Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeya City yavunja uteja ikiikamua Mashujaa Sokoine

MBEYA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi nne walizokutana hapo kabla, Mashujaa imeshinda zote na leo Mbeya City imevunja uteja dhidi ya wapinzani hao, huku ikivuna pointi sita katika mechi tatu ilizocheza nyumbani na kuwa nafasi ya nne kwa pointi sita. 

Licha ya kutangulia kupata bao, Mashujaa imejikuta katika kibano baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu Bara. 


Hata hivyo, matokeo hayo yanamaliza kiu ya Mbeya City iliyosota kwa muda mrefu kupata ushindi dhidi ya Maafande hao katika michezo minne waliyokutana hapo kabla. 

Ikumbukwe Mashujaa ilipanda Ligi Kuu misimu miwili iliyopita kupitia play off kufuatia matokeo ya jumla ya mabao 3-1 dhidi ya wapinzani hao na kuwashusha daraja katika Uwanja wa Sokoine. 

Katika mchezo wa leo, Mashujaa ndio walitangulia kupata bao dakika ya 65 kupitia kwa Hija Shamte, kabla ya Mbeya City kusawazisha kwa penalti kupitia Adil Buha.

MBE 01

Mabadiliko ya kiufundi kwa Mbeya City kuwaingiza Aziz Kada na Oscar Mwajanga waliopishana na Vitalis Mayanga na Willy Mwani, yalikuwa na faida yaliyowapa bao la pili kupitia kwa Mwajanga na kudumu hadi dakika 90.

Huo unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Mbeya City baada ya ule wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji, huku Mashujaa ikipoteza wa pili mfululizo baada ya kutoka kuchapwa na Fountain Gate. 

MBE 02

Huu ni mchezo wa tatu mfululizo kwa Mbeya City kucheza nyumbani huku Mashujaa wakicheza pia dakika 270 ugenini na sasa Mbeya City itatoka kuwafuata Fountain Gate huku Mashujaa wakiwa nyumbani kuipokea Kagera Sugar. 

Kocha Mkuu wa Mashujaa, Aman Josiah, amesema matokeo hayo si mazuri kwao akieleza kuwa wanahitaji kujiandaa bila ya kujali mechi za nyumbani au ugenini. 

MBE 03

"Kisaikolojia hatukuwa sawa, safari nazo zinachangia lakini hakuna namna zaidi ya kupambana kutafuta ushindi kwa mechi zijazo bila kujali nyumbani au ugenini," amesema Josiah.