Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Matheo ashikiria rekodi SportPesa

Dar es Salaam: Hadi timu zinakwenda hatua ya fainali ya mashindano ya SportPesa, mshambuliaji wa Yanga, Matheo Anthony ndiye mchezaji pekee kutoka Tanzania aliyefunga bao ndani ya dakika 90 za mchezo katika michuano hiyo.

Matheo ambaye kikosi chake kilitolewa hatua ya robo fainali na Kakamega, alifunga bao hilo  kwa njia ya faulo iliyokwenda moja moja wakati timu yake ilipokula kichapo cha mabao 3-1.

Simba ambayo imeingia fainali baada ya kuifunga  Kariobang Sharks kwa penalti pia iliichapa Kakamega Homeboyz hatua nusu fainali kwa penalti, iko hivyo pia kwa Singida ambayo sasa iko uwanjani inakipiga na Gor Mahia.