Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Malindi kurejea Unguja na pointi tatu za Chipukizi

MLANDEGE Pict

Muktasari:

  • Bao hilo lilifungwa na Tchakei Moucheri dakika 15 akimalizia pasi ya Ramadhan Mponda ambapo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.

TIMU ya Malindi kutoka Unguja, imefanikiwa kuvuna alama tatu kwa kuifunga Chipukizi bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu Zanzibar iliyochezwa Septemba 27, 2025 kwenye Uwanja Gombani uliopo kisiwani Pemba.

Bao hilo lilifungwa na Tchakei Moucheri dakika 15 akimalizia pasi ya Ramadhan Mponda ambapo lilidumu hadi timu hizo zinakwenda mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa Chipukizi kupambana kusawazisha bao hilo, lakini ilishindwa kufanikisha hilo na kujikuta ikianza ligi kwa kichapo cha nyumbani.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Msaidizi wa Malindi, Mohamed Salah 'Richkard' amesema mechi hiyo ilikuwa ngumu lakini wachezaji walijituma vya kutosha kuhakikisha wanapata ushindi.

MLAND 01
MLAND 01

Richkard amesema mambo yote ambayo walikuwa wanayafanyia kazi uwanja wa mazoezi ndiyo yaliyorahisisha kuibuka na ushindi huo, hivyo hilo ni jambo la faraja upande wao.

Timu hizo huo ulikuwa ni mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu Zanzibar iliyoanza Septemba 25, 2025.