Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Makipa Dodoma Jiji mh!

HUKO Dodoma Jiji makipa wake wametoa kali baada ya wote watatu kujifunga mabao ya aina moja ya kusukumizia mipira wavuni katika mechi tatu tofauti kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu.
Makipa hao wakiwa kwenye harakati za kuokoa mipira ya mbali wameonyesha hawapo makini baada ya kila mmoja kukubali kuruhusu bao la mbali kwa kujifunga.
Hussein Masalanga ndiye aliyekuwa kipa wa kwanza kujifunga kwenye mchezo wao dhidi ya Mbeya City (mzunguko wa kwanza) baada ya kupigwa kona na Selemani Ibrahim iliyoenda moja kwa moja kwenye boksi lakini Masalanga wakati anaucheza mpira huo mbele yake kulikuwa na kiungo wake Salmin Hoza na kumfanya mpira aupangue ndani ya boksi.
Kipa wa pili kujifunga ni Rahim Sheikh kwenye mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar uliochezwa Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kipa huyo alishindwa kupiga hesabu zake vizuri alipokuwa anadaka krosi ya Baba Ubaya ambaye mpira wake ulikuwa na kasi na wakati Rahim alipotaka kuudaka ulimzidi mikononi na kuudondosha chini na moja kwa moja ulienda wavuni.
Kipa wa tatu aliyejifunga ni Mohamed Yusuph ambaye aliingia mchecheto baada ya kucheza shuti la nje ya boksi lililopigwa na Zawadi Mauya wa Yanga na mpira ulipokuwa angani huku washambuliaji Fiston Mayele na Dickson Ambundo walipokuwa karibu yake alionekana kupagawa na kuudumbukiza mwenyewe mpira wavuni.
Kwa matukio hayo ya makipa, kocha wao wa makipa Adam Abdalah ‘Meja’ alisema kwa kosa la kipa wake Mohamed alitakiwa kutumia mbinu za makipa katika mipira kama ile kwa sababu kanuni zipo.
“Mbinu za makipa kucheza mipira ya namna ile zipo lakini naona yeye aliamua kufanya ambacho kilikuwa kichwani kwake kwa wakati ule, sio yeye hata makipa wa timu zingine kuna muda hufanya tofauti na wanachoelekezwa,” alisema Meja.
“Sisi kazi yetu ni kama makocha unamfundisha mwanafunzi, kutambua makosa wanayofanya na kuyafanyia kazi hivyo tutaendelea kurekebishana.”