Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lagrouni aanza kibabe kuwapika mastaa Yanga

Muktasari:

  • Taibi Lagrouni  amekuja kuchukua nafasi ya Helmy Gueldich 'Manywele' ambaye Mwanaspoti linafahamu hataweza kurejea katika timu hiyo, jamaa katika mazoezi yake ya siku mbili tu ameanza kwa kishindo akiwakimbiza wachezaji asubuhi kisha jioni ratiba hiyo inabadilika.

KIKOSI cha Yanga kinaendelea kujifua katika kambi ya timu hiyo iliyopo Avic Town, Kigamboni chini ya kocha mpya, Miguel Gamondi lakini taarifa mpya ni kwamba kocha huyo kutoka Argentina ameshusha mtaalamu mwingine aliyeanza kazi ya kibabe kuwapika mastaa wa timu hiyo kambini.

Mtaalamu huyo mpya ametua Yanga na ametambulishwa jana usiku ikiwa ni siku chache tangu klabu hiyo imlete Kocha Msaidizi Moussa N'Daw kutoka Senegal na kusajiliwa kwa nyota watano waliotambulishwa Jonas Mkude, Maxi Nzengeli, Gift Fred, Nickson Kibabage na Kouassi Yao.

Taibi Lagrouni  amekuja kuchukua nafasi ya Helmy Gueldich 'Manywele' ambaye Mwanaspoti linafahamu hataweza kurejea katika timu hiyo, jamaa katika mazoezi yake ya siku mbili tu ameanza kwa kishindo akiwakimbiza wachezaji asubuhi kisha jioni ratiba hiyo inabadilika.

Kumekuwa na ratiba ngumu katika mazoezi ya asubuhi ambapo kiwango kikubwa kinakuwa ni kujaza fiziki na pumzi ya mwili kabla ya jioni Gamondi kuingia kazini akiwa na N'Daw.

Ratiba ya jioni Gamondi huingia kazini na N'Daw ambapo ratiba ya mazoezi ya kucheza soka uwanjani yanafanyika ambapo makocha hao wamekuwa wakitaka kuona falsafa ya timu kucheza soka la pasi nyingi na kujua kukaba inaingia katika vichwa vya wachezaji hao.

Kambi hiyo jan ilianza kuwapokea wachezaji wao wapya wengine wawili ambao walikuwa hawajaanza mazoezi ambao ni beki Kouassi Yao na winga Maxi Nzengeli.

Wachezaji watatu wapya pekee ambao walikuwa wameshaanza mazoezi hayo ni beki Nickson Kibabage, beki Gift Fred na kiungo Jonas Mkude ambao wiki hii wataingia kwenye wiki ya pili ya mazoezi hayo, huku mabosi wakiendelea kuchekecha majina yaliyosaliwa wa kusajiliwa kikosini.

Yanga inasaka straika ika mpya baada ya kumalizana na Fiston Mayele anayejiandaa kutimka kati ya Pyramids ya Misri na klabu ya Al Qadisiyah ya Saudi Arabia anayoichezea Simon Msuva.