Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha mpya Mtibwa Sugar abebeshwa matumaini kubakisha Ligi Kuu

Kocha Mpya wa Mtibwa Sugar, Mohamed Badru akiongea na waandishi wa habari baada ya kuanza kazi rasmi ya kukinoa kikosi hicho na mchezo wake wa kwanza kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika uwnaja wa Jamhuri Morogoro, Picha na Juma Mtanda.

Muktasari:

Kocha Mohamed Badru ametua kiroho ngumu katika klabu ya Mtibwa Sugar kutokana na matokeo mabaya ya ligi kuu Tanzania bara lakini mchezo wake wa kwanza ameweza kuibua na ushidi wa bao 2-0 dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa jamhuri Morogoro.

Klabu ya Mtibwa Sugar imeeleza kuwa wamefanya mabadiliko ya gafla ya kusaka kocha wa kukinoa lakini kukinusuru na janga la kushuka daraja kutokana na mwenendo mbaya wa michezo ya ligi kuu Tanzania ikiwa ilijiweka katika hatari ya timu kushusha mkoani hapo.

Akizungumza na Mwanaspoti katika mahojiano maalumu mkoani hapa, Msemaji wa klabu hiyo, Thobias Kifaru alisema kuwa timu ilikuwa katika hatihati ya kushuka kutokana na mwenendo mbovu na kuwalazimu kufanya maamuzi magumu ya kusaka kocha wa kurekebisha hali hiyo.

Kifaru alisema kuwa tayari wamemsainisha, Mohamed Badru kuwa kocha mkuu wa miamba hiyo akichukua mikopa ya, Heri Ndalaigije aliyeachana na timu hivi karibuni.

“Tumejeresha umoja, mshikamano na katika michezo miwili dhidi ya Tanzania Prison na Mbeya City kutoka jijini imetuwafanya tupumua baada ya kukusanya alama 34 tukiendelea kukimbia katika mbaya za kushuka daraja na tumemsainisha kocha, Mohamed Badru kuongeza nguvu.’alisema Kifaru.

“Mkosi ulianza zaidi kutuandama baada ya aliyekuwa kocha wetu mkuu, Zuberi Katwira kutimukia Ihefu Fc na timu kuwa chini ya Vicent Barnabas tukaendelea kufanya vibaya na kuwa na kocha……….aliyetimukia wao Burundi na sasa tunaye, kocha mwenye heshima kubwa Tanzania, Mohamed Badru ambaye kwa sasa ndio tunamtegemea kuituliza timu na kuweka mipango sawa msimu ujao.”alisema Kifaru.

Aliongeza kuwa baada ya wachezaji wa zamani wa klabu hiyo wamelazimika kujikusanya na kukaa na wachezaji kuwaongezea morali ili timu hiyo iweke kubaki ligi kuu na wachezaji hao kuahidi kuambatana na timu kila itakapoenda kwa michezo iliyosalia.

Kabla ya michezo hiyo, Mtibwa ilikuwa kwenye hatari ya mstari mwekundu ikiwa na alama 29 katika msimamo ikiwa ya pili kutoka chini na ushindi dhidi ya Prison wa bao 1-0 na leo dhidi ya Mbeya City wa bao 2-0 umepunguza presha kwao baada ya kuweka kibindoni alama 34 ikiwa katika nafasi ya 11 ya msimamo wa ligi kuu.

Kwa upande wa Kocha mkuu wa Mtibwa Sugar, Mohamed Badru alisema ameshukuru kwa wachezaji kumpa heshima katika mchezo wake wa kwanza kupata ushindi mbele ya Mbeya City wa bao 2-0 katika uwanja wa jamhuri Morogoro.

“Nimepokelewa vizuri na viongozi, wachezaji na wapenzi wa soka Morogoro kwa mchezo wangu wa kwanza kupata ushindi wa bao 2-0 mbele ya wapinzani wetu na hii inanifanya kuongeza mbinu katika michezo iliyobaki ili tuweze kupata ushindi na lengo letu sote ni kuhakikisha tunaungana kuwa kitu kimoja ili kupata ushindi.’alisema Badru.

Badru alisema amekaa na wachezaji siku mbili kabla ya mchezo lakini akawataka kutumia mbinu ya kushambulia na wasijilinde kwa sababu kuna kitu walikuwa wanatafuta na kupata mabao mawili yaliyowafanya wapunguze presha.

“Mwandishi unaweza kuona Mtibwa imebadiliko katika mchezo wetu na Mbeya City na wachezaji walikosa vitu vya kisaikolojia na kukosa utulivu wa akili ikiwemo nidhamu na kwa sababu tutakuwa na mapumziko tukirejea timu itakuwa na mabadiliko makubwa na nimekuwa kwa kazi moja ya kubakisha timu ligi kuu.”alisema Badru.