Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo Yanga atibua usajili wa Mo Simba

Muktasari:

  • Kufuatia taarifa hizo Mwanaspoti lilimtafuta Raoul Shungu ambaye alithibitisha kusikia ishu ya Yanga kumhitaji Mundele lakini akasema mambo kamili yatafanyika mara timu yao itakapotua nchini.

KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kurejea nchini leo Jumanne Alasiri kikitokea Algeria, kilipoenda kuchezea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wenyeji wao, JS Saoura katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini kabla haijaondoka mabosi wao walikuwa wakipiga hesabu kali ya kusajili jembe jipya.

Simba ilikuwa kwenye mipango ya kufanya usajili mmoja mkubwa wa straika anayesumbua katika kikosi cha AS Vita ambao watavaana nao Jumamosi hii, lakini ghafla ikaelezwa Wamorocco nao wametia miguu wakitaka kumchukua mwishoni mwa msimu huu.

Lakini sasa unaambiwa upepo umebadilika baada ya kigogo mmoja wa Yanga na mtu mwenye fedha zake kuamua kupiga simu DR Congo na akitaka kumchukua juu kwa juu mshambuliaji huyo matata.

Kwani mnafikiri straika huyo ni nani babi? Ni Makusu Mundele anayeiongoza safu ya ushambuliaji ya Vita ambapo chini ya bilionea wake Mohammed ‘MO’ Dewji, Simba alivutiwa na straika huyo na kuuliza bei yake.

Harakaharaka mshambuliaji huyo akawaambia Simba waandae kiasi kisichopungua Sh. 250 milioni ili waanze mazungumzo na makubaliano yangekuwa mwishoni mwa msimu.

Yanga nayo wakapitia mlango wa uani kuhitaji saini ya Mundele wakimtumia kocha wao, Mwinyi Zahera kuweka mambo sawa akiwasiliana na kocha aliyewahi kuinoa Yanga miaka ya nyuma, Raoul Shungu.

Tajiri huyo (jina tunalo) amemsuka vyema Shungu na kwamba mara AS Vita itakapotua nchini kikao cha siri kitafanyika kujipanga vyema dili hilo.

Walichovujishiwa Yanga ni kwamba klabu ya Morocco inayomtaka Mundele imeonyesha nia tu ya kumsajili mshambuliaji huyo lakini haijafanya lolote kubwa katika kujihakikishia dili hilo.

Mbali na hilo, Yanga imeambiwa mkataba wa mshambuliaji huyo uko mwishoni na kama akimaliza mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, basi anatakuwa huru.

Kufuatia taarifa hizo Mwanaspoti lilimtafuta Raoul Shungu ambaye alithibitisha kusikia ishu ya Yanga kumhitaji Mundele lakini akasema mambo kamili yatafanyika mara timu yao itakapotua nchini.

Shungu alisema, Yanga itakutana na mabosi wa Vita katika kikao cha kuzungumzia dili hilo.

“Yanga wanamtaka Mundele kama hao Simba, lakini nafikiri kutakuwa na kikao tukifika huko Tanzania,” alithibitisha Shungu.

Straika huyo anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji wa AS Vita watakaokuja nchini kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Kundi D kati yao na Simba utakaopigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa kuanzia saa moja usiku ambapo mshindi atakata tiketi ya kwenda kucheza kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.