Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamati kuamua ishu ya straika Simba

Mnuka Pict
Mnuka Pict

Muktasari:

  • Agosti Mosi, mwaka huu, Mwanaspoti iliripoti nyota huyo wa timu ya taifa (Twiga Stars) ametoroka kambini ikiwa ni siku chache tangu atoke kwenye majukumu ya taifa.

BADO sakata la mshambuliaji Aisha Mnunka na klabu yake ya Simba halijamalizika na sasa kamati ya hadhi za wachezaji itakutana kumaliza ishu hiyo.

Agosti Mosi, mwaka huu, Mwanaspoti iliripoti nyota huyo wa timu ya taifa (Twiga Stars) ametoroka kambini ikiwa ni siku chache tangu atoke kwenye majukumu ya taifa.

Hata hivyo, baada ya sakata hilo, baadae Simba Queens ilitoa ripoti nyota huyo aliondoka kambini bila ruhusa na wamepeleka kesi Shirikisho la Soka nchini (TFF) juu ya kutoonekana klabuni kwa mchezaji wao.

Mwanaspoti lilimtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji, Said Soud na alisema kesi hiyo ipo na kabla ya Novemba 20, mwaka huu itakuwa imesikilizwa.

"Bado hatujajua vizuri kama Simba wamepeleka barua, lakini ni kesi ambayo iko 'pending' na kabla ya Novemba 20 kama kamati tutakuwa tumekutana na kujua muafaka juu ya jambo hilo," alisema Soud na kuongeza;

"Kuhusu mchezaji pia hatujapata barua kwa sababu sisi hatuhusiki, lakini kama nilivyosema hilo shauri lipo na kamati itaamua, kwa sasa hatuwezi kuliongelea sana."