Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hersi: Ngao ya Jamii ya Yanga yaibwa, awataka walioichukua wairudishe

NGAO Pict

Muktasari:

  • Kauli hiyo iliibua mshangao miongoni mwa wanachama waliohudhuria mkutano huo, huku wengi wakitaka waliohusika na wizi huo wachukuliwe hatua na kuhakikisha taji hilo linapatikana.

Rais wa Yanga, Injinia Hersi Said, ametoa taarifa iliyowashtua wanachama wa klabu hiyo baada ya kufichua kuwa taji la Ngao ya Jamii walilotwaa mwaka 2025 limeibwa.

Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Yanga, Hersi alisema wakati uongozi ukiwa unawasilisha mataji mbalimbali yaliyotwaliwa msimu uliopita, walilazimika pia kutoa taarifa ya kupotea kwa moja ya makombe muhimu ya klabu.

"Ndugu zangu, wakati tunawaletea mataji tuliyoyashinda msimu uliopita, kuna habari mbaya nataka kuwapa," alisema Hersi.

Aliongeza kuwa taji la Ngao ya Jamii walilotwaa mwaka 2025 liliibwa katika mazingira yaliyowashtua viongozi wa klabu hiyo.

"Wakati tunasherehekea mataji yetu, jambo la kushangaza kuna mtu alituibia taji la Ngao ya Jamii tulilochukua mwaka 2025. Tumesikitishwa na tukio hilo na hadi sasa hatujui lilipo," alisema.

Hersi aliwataka waliohusika na tukio hilo kulirudisha mara moja, akisisitiza kuwa kombe hilo lina thamani kubwa kwa historia ya klabu.

Wakati huo huo, alisema Yanga tayari imeanza kuchukua hatua za kupata taji jingine kwa kushirikiana na mamlaka za soka nchini.

"Tayari tumeshawasiliana na mamlaka husika ili tutengenezwe Ngao nyingine. Mtengenezaji wa kombe hilo alikuwa Mtanzania na mchakato wa kutengeneza jingine tayari umeanza," alisema Hersi.

Kauli hiyo iliibua mshangao miongoni mwa wanachama waliohudhuria mkutano huo, huku wengi wakitaka waliohusika na wizi huo wachukuliwe hatua na kuhakikisha taji hilo linapatikana.