Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Frank Lampard kupewa miaka mitatu safi Chelsea

Muktasari:

Lampard aliifikisha Derby hatua ya mtoano kupanda Ligi Kuu ya England ambapo, nusura ipande daraja lakini ikachapwa 2-1 na Aston Villa katika pambano la fainali lililofanyika Uwanja wa Wembley.

LONDON,ENGLAND.MDAKU mmoja amedai ana uhakika kuwa tajiri wa Chelsea, Roman Abramovich amempa kazi kiungo wa zamani wa klabu hiyo, Frank Lampard kuwa kocha kwa mkataba wa miaka mitatu.

Lampard, 40, ndiye anaongoza katika mbio za kumrithi kocha Maurizio Sarri, ambaye ameachana rasmi na klabu hiyo na kutangazwa kuwa kocha wa Juventus kuanzia msimu ujao.

Nicolo Schira, mwandishi mzoefu wa gazeti maarufu la michezo la Italia, Gazzetta dello Sport amedai ana habari za ndani kuwa Lampard amepewa mkataba wa miaka mitatu kuwa kocha mpya wa Chelsea kuanzia msimu ujao.

Lampard alikutana na Abramovich katika boti yake ya kifahari St Tropez kule Ufaransa wiki iliyopita wakati tajiri huyo akiwa likizo na amempa kazi ya kurudisha heshima ya Chelsea.

Lampard alikuwa na hofu kuchukua kazi hiyo kutokana na tabia ya Abramovich kuwafukuza makocha, lakini tajiri huyo wa Kirusi amemhakikishia kuwa atampa miaka miwili ya kwanza ya kufanya kazi bila ya kufukuzwa hata kama matokeo hayatakuwa mazuri. Kuna shaka miongoni mwa mashabiki wa Chelsea kwamba, Lampard hana uzoefu wa kutosha kuhimili mikikimikiki ya Ligi Kuu ya England licha ya kufanya vema katika msimu wake wa kwanza kama kocha akiwa na klabu ya Derby County ya Ligi Daraja la Kwanza.

Lampard aliifikisha Derby hatua ya mtoano kupanda Ligi Kuu ya England ambapo, nusura ipande daraja lakini ikachapwa 2-1 na Aston Villa katika pambano la fainali lililofanyika Uwanja wa Wembley.

Derby haina kinyongo kwa Lampard kurudi Stamford Bridge kama kocha, lakini lazima italipwa kiasi kikubwa cha pesa kama fidia kutokana na kuwa na mkataba na kocha huyo, ambaye wangependa aendelee kuwepo kikosini kwao.

Uvumi umeanza kutanda kuwa huenda Lampard akamchagua straika nyota wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba aliyecheza naye kwa mafanikio Stamford Bridge kuwa msaidizi wake.

Kwa upande wake, Drogba amekaririwa akiupigia debe uteuzi wa Lampard kuwa kocha mkuu wa Chelsea huku akidai alijua mapema kiungo pamoja na staa mwingine wa zamani wa Chelsea wangekuwa makocha wazuri siku za usoni.

“Hawa wawili walikuwa uti wa mgongo wa timu kwa zaidi ya muongo mmoja. Wametufanyia mambo makubwa pale Chelsea. Uliponiambia huo ni mwelekeo (Lampard) anataka kuuchukua nilijua angefanya mambo makubwa kwani, ana ubora ambao unatakiwa. Anasikiliza, ni mshindi, anafanya sana kazi kama John alivyokuwa. Wote wawili ni watu wazuri na wanapiga mzigo,” alisema Drogba.

Endapo atarudi klabuni hapo, Lampard atapokewa kama shujaa na mashabiki wa Chelsea ambao, bado wanamhusudu huku rekodi yake ikiwa wazi kabuni hapo na anabakiwa kuwa mmoja kati ya wachezaji wenye mafanikio.

Aliwahi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea mara tatu huku akiwa mfungaji bora wa muda wote katika historia ya Chelsea, ambapo alifunga mabao 211 katika michuano mbalimbali tangu alipojiunga klabuni hapo mwaka 2001 akitokea West Ham.

Lampard ni mmoja kati ya wachezaji saba katika Ligi Kuu ya England waliofunga mabao 150 au zaidi huku katika orodha hiyo yeye akiwa yeye ndiye kiungo pekee.

Katika orodha ya wachezaji waliopika mabao mengi kwa wenzao katika Ligi Kuu ya England anashika nafasi ya nne akiwa na pasi za mabao 102.