Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dante alianzisha mapema huko Yanga

Muktasari:

Fatas mabeki wanne wametua Jangwani akiwamo Lamine Moro, Ali Ali, Seleman Mustafa na Ally Mtoni ‘Sonso’ mbali na viungo, mawinga na washambuliaji, jambo lililomfanya Dante kuamini Yanga ya msimu ujao itatisha na kusumbua sana.

Dar es Salaam. Mabosi wa Yanga wameendelea kumwaga fedha kuhakikisha wanasuka kikosi chao ili kushindana vilivyo kwenye michuano itakayoshiriki msimu ujao, huku beki wake wa kati, Andrew Vincent ‘Dante’ akilianzisha mapema akidai wapinzani wakae chonjo.
Ipo hivi. Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera tayari alishawapa mabosi wake majina ya nyota anaowataka na kweli wamekuwa makini kuhakikisha wanatua Jangwani na Mwenyekiti Dk. Mshindo Msolla amekuwa akikaririwa akidai hawataacha anayetakiwa.
Fatas mabeki wanne wametua Jangwani akiwamo Lamine Moro, Ali Ali, Seleman Mustafa na Ally Mtoni ‘Sonso’ mbali na viungo, mawinga na washambuliaji, jambo lililomfanya Dante kuamini Yanga ya msimu ujao itatisha na kusumbua sana.
Dante alisema kwa kuongezewa nguvu kwa beki ya kati ni jambo zuri kuhakikisha watakuwa hawaruhusu kupitwa kizembe na kuamini wale waliokuwa wameigeuza Yanga chochoro kupata ushindi kwao wajipange kweli kweli la sivyo wataumia.
“Wote waliosajiliwa ni wazuri, kwani tulikuwa tukiwaona wanavyocheza, washambuliaji wa timu pinzani watambue haitokuwa rahisi kwao kutupita na kutufunga,” alisema Dante aliyetua misimu mitatu iliyopita akitokea Mtibwa Sugar.
Akizungumzia kwa upande wa changamoto ya namba alisema jambo hilo litakuwa na ushindani mkubwa lakini lengo ni moja tu kuhakikisha timu inafanya vizuri.
“Changamoto itakuwepo hilo kila mmoja mpaka hivi sasa   ameshaona, lakini kikubwa ni kufanya mazoezi vizuri na mwalimu ndio ataamua nani acheze kulingana na mahitaji yake,” alisema.
Aliongeza changamoto hiyo itafanya kila mchezaji kujituma zaidi anapokuwa uwanjani kwani anajua akikosea basi mwenzake atachukua nafasi.
“Ukipata nafasi inabidi uitumie vizuri kwelikweli, sasa hapo ndio washambuliaji wa timu pinzani watakapokuwa wanakutana na changamoto nyingine,” alisema.
Mbali na mabeki, Yanga pia imesajili washambuliaji watano ambao ni Maybin Kalengo, Sadney Urikhob, Issa Bigirimana, Patrick Sibomana na Juma Balinya mbali na viungo Mapinduzi Balama na Abdulaziz Makame.