Chilambo aanza vitisho Stars
Muktasari:
- Taifa Stars tayari imepata tiketi ya AFCON 2027 kutokana na Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa mashindano hayo, lakini bado inaendelea na ratiba ya mechi za kufuzu kama sehemu ya mch akato wa maa nda lizi ya kikosi hicho.
BEKI wa Simba, Nathaniel Chilambo amesema mechi za kufuzu AFCON 2027 ambazo Taifa Stars itacheza dhidi ya Guinea Bissau na Madagascar haziwezi kuchukuliwa kama burudani kwa sababu kila mechi ni sehemu ya maandalizi ya Tanzania kwa ajili ya fainali hizo zitakazofanyika Afrika Mashariki.
Taifa Stars tayari imepata tiketi ya AFCON 2027 kutokana na Tanzania kuwa mwenyeji mwenza wa mashindano hayo, lakini bado inaendelea na ratiba ya mechi za kufuzu kama sehemu ya mch akato wa maa nda lizi ya kikosi hicho.
Chilambo alisema hali hiyo haimaanishi wachezaji wanaingia uwanjani kwa ajili ya kutimiza ratiba, bali wanapaswa kutumia kila mchezo kutafuta matokeo na kumpa kocha, Miguel Gamondi nafasi ya kubaini maeneo yanayohitaji maboresho.
“Hatutacheza kama kujifurahisha. Tunacheza kwa ajili ya kupata matokeo katika kila mchezo ili kuangalia tunafanya vipi kuelekea kwenye mashindano ambayo yatakuwa kwenye ardhi yetu ya nyumbani, tujue tuko katika nafasi gani na mwalimu aangalie eneo gani lina tatizo ili azidi kurekebisha,” alisema Chilambo.
Beki huyo alisema mechi hizo ni muhimu pia kwa wachezaji kwa sababu zinawapa nafasi ya kuelewa zaidi falsafa ya kocha na kujenga kikosi kitakachokwenda kushindana katika mashindano makubwa.
“Ukisema tunaenda kucheza kwa ajili ya kujifurahisha, maana yake mwalimu atakuwa hajapata kile ambacho anakikusudia kwa ajili ya kuelekea kwenye mashindano makubwa yanayokuja,” alisema.
Chilambo ambaye amekuwa kwenye kiwango bora kwa sasa tangu ajiunge na Simba akitokea Azam FC, alisema kuitwa kwake Taifa Stars kumempa faraja kubwa kwa sababu ni ndoto ya kila mchezaji kupewa nafasi ya kuwakilisha nchi yake na kupigania mamilioni ya Watanzania wanaoiunga mkono timu hiyo.
Alisema kiwango chake Simba ndicho kilichomsaidia kupata nafasi hiyo, akimtaja kocha Gamondi, ameona kile alichokuwa akikifanya katika klabu yake na kumpa nafasi ya kuja kuongeza nguvu kwenye timu ya taifa.