Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chidale ashinda Tanzania Open 2026

CHIDALE Pict

Muktasari:

  • Chidale alikusanya mikwaji 73 katika siku ya kwanza na baadaye kusanya mikwaju 69 katika siku ya pili na mikwaju mingine 69 katika siku ya tatu na mikwaju 78 katika siku ya nne kutwaa zawadi ya kwanza ya Sh 9.35 milioni kutoka kwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo.

KAMA sehemu ya dhamira yake ya kuendeleza michezo, kukuza vipaji vya Watanzania na kujenga majukwaa yanayounganisha wadau wa michezo na biashara, Vodacom Tanzania Plc kupitia Vodacom Business imeendelea kudhamini mashindano ya gofu, ambayo mwaka huu yamefikia kilele      na  mchezaji raia wa Malawi, Paul Chidale ameweka rekodi kwa kusanya jumla ya mikwaju 289 kwenye Uwanja wa Kili Golf mkoani Arusha.

Chidale alikusanya mikwaji 73 katika siku ya kwanza na baadaye kusanya mikwaju 69 katika siku ya pili na mikwaju mingine 69 katika siku ya tatu na mikwaju 78 katika siku ya nne kutwaa zawadi ya kwanza ya Sh 9.35 milioni kutoka kwa wadhamini wakuu wa mashindano hayo.

Nafasi ya ushindi wa pili ilikwenda kwa Mtanzania Nuru Mollel, kwa kukusanya mikwaju 293 na mchezaji wa Kenya,  Robinson Owiti alimaliza  nafasi ya tatu kwa mikwaju 294.

Mashindano hayo ya siku nne, yaliyofanyika kuanzia Oktoba 22 hadi 25 katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha, yaliwakutanisha wachezaji wa golf kutoka Tanzania na nchi mbalimbali, yakitoa jukwaa la ushindani wa kiwango cha juu, maendeleo ya vipaji na kuimarisha mchango wa mchezo wa golf nchini.

Akizungumza katika hafla ya kufunga mashindano hayo, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, amesema kampuni hiyo inatambua nafasi ya michezo katika kuunganisha watu huku ikikuza vipaji na kufungua fursa za ushirikiano na uhusiano.

“Tunatambua nafasi ya michezo katika kuunganisha watu, kukuza vipaji na kufungua fursa mpya za uhusiano na ushirikiano. Tunaunga mkono majukwaa kama Vodacom Tanzania Open yanayochangia kuendeleza mchezo wa golf nchini, kuwapa wachezaji fursa ya kuonyesha uwezo wao na kuwakutanisha wadau wa michezo na biashara. Kwetu, huu ni sehemu ya kutimiza ahadi yetu ya zaidi ya Mtandao kwa kujenga mahusiano yenye thamani na kuchangia maendeleo ya jamii na sekta mbalimbali.”

Hafla ya hiyo ilihusisha makabidhiano ya vikombe na zawadi za fedha kwa washindi. Katika kundi la wachezaji wa kulipwa, mshindi wa kwanza alijishindia Sh9.35 milioni, wa pili Sh6.35 milioni na wa tatu Sh4.35 milioni kati ya jumla ya Sh40 milioni zilizotolewa kwa washindi mbalimbali. Mwenyekiti wa chama cha Gofu Tanzania (TGU), Gilman Kasiga, aliipongeza Vodacom huku akisema imeleta nafasi muhimu katika maendeleo ya golf nchini.

“Vodacom Tanzania Open ni jukwaa muhimu kwa maendeleo ya golf nchini, kwani linawapa wachezaji fursa ya kupima uwezo wao katika ushindani wa kiwango cha juu na kujifunza kutoka kwa wachezaji wengine.”

Akizungumzia ushindi wake, Chidale amesema kwamba ushindi huu una maana kubwa kwake kwa sababu amepitia katika ushindani mkali kutokana na aina ya washiriki waliokuwepo.

“Kushinda mashindano haya kuna maana kubwa kwangu. Ushindani ulikuwa mkali, na ushindi huu unaakisi bidii na maandalizi yaliyohitajika ili kufanya vizuri katika kiwango hiki. Nawashukuru waandaaji na wadhamini kwa kuwezesha mashindano haya, yanayowapa wachezaji mahiri kutoka maeneo mbalimbali fursa ya kukutana na kushindana,” amesema Chidale.