Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama aukubali mziki wa Azam, asema kazi ipo

KIUNGO wa Simba, Clatous Chama 'Tripple C' amesema kuwa msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara utakuwa na ushindani kutokana na jinsi wachezaji wapya wanaosajiliwa.

Chama ameyasema hayo wakati akizungumza kwenye mtandao wa Instagram akiwa live na ametoa nafasi kubwa kwa matajiri wa Jiji la Dar es Salaam Azam FC, kufanya vizuri kutokana na usajili wanaoendelea kuufanya mpaka sasa.

Nyota huyo alisema wachezaji wapya wanaosajiliwa na uongozi wa timu hiyo chini ya kocha Mzambia George Lwandamina anaiona timu hiyo ikitengeneza timu bora kwa ajili ya kuleta ushindani msimu ujao.

"Natumaini usajili unaofanyika na Azam ni dhahiri utaleta ushindani mkubwa msimu ujao kwenye Ligi, lakini pia itakuwa poa kuona Azam ikishinda kwa ajili ya mataji na vyote unajua tusiwe tu na Ligi ya Simba na Yanga, mara hii nadhani azam FC wamesajili vizuri" alisema.

Chama alisema kuwa wachezaji wengi wanaosajiliwa na kikosi hicho anawajua na anadhani watajenga timu bora watakapokuwa na muunganiko, huku akitoa rai kuwa viongozi wanapaswa kuwa makini kwenye usajili kwani wanaweza wakasajili wachezaji wapya lakini timu ikashindwa kuwa na muunganiko mzuri.

"Suala la muunganiko ni nzuri kwenye timu na unajua siyo tu suala la usajili, kwani hapa ndipo inabidi tuwe waangalifu sana kwani unaweza ukafanya usajili mpya lakini timu ikawa haina muunganiko halafu ikawa tatizo," alisema.

Azam FC mpaka sasa imenasa saini ya wachezaji saba kuelekea msimu ujao ambao ni golikipa, Ahmed Ali Suleiman 'Salula' kutoka KMKM ya Zanzibar, beki wa kushoto, Edward Manyama, kiungo mkabaji, Paul Katema (Zambia), viungo washambuliaji, Charles Zulu (Zambia), Kenneth Muguna (Kenya) na washambuliaji Rodgers Kola (Zambia) na Idriss Mbombo (DRC).

IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI