Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Chama afunguka ishu ya Luis, aanika mipango yake Simba

KIUNGO fundi wa mpira wa Simba, Clatous Chama 'Tripple C' ameeleza hisia zake juu ya sakata linalomhusisha winga wa timu hiyo, Luis Miquisonne anayehusishwa kujiunga na Al Ahly ya Misri.
Taarifa zinadai nyota huyo amewaaga marafiki zake wa karibu kwa ajili ya kujiunga na mabingwa hao wa Afrika, huku Chama akisema kuwa yeye hausiki chochote kwenye kumshawishi nyota huyo kubakia Simba.
"Ni juu yake Luis Miquisonne kuchagua kama ataondoka au atasalia Simba. Mimi ni rafiki yake, hivyo nitamshauri aangalie sehemu anayoona kwake kunafaa na kama akiamua kuondoka nitamuunga mkono na kama akitaka kubaki nitamuunga mkono pia" alisema Chama ambaye msimu huu akishirikiana na Luis walitengeneza mabao zaidi ya 30 wakifunga na kuasisti.
Inaelezwa Luis amesajiliwa nma Al Ahly kwa dau la Dola 900,000 (zaidi ya Sh2 Bilioni) ikiwa ni misimu miwili tu tangu asajiliwe kutoka UD Songo ya Msumbiji alikokuwa akiichezea kwa mkopo kutoka Mamelodi Sundwons ya Afrika.
Winga huyo ambaye awali alikuwa njiani kutua Jangwani kabla ya Simba kufanya umafia na kumkomba juu kwa juu, amemaliza msimu uliopita akifunga mabao tisa na kuasisiti 10, huku Chama akiwa kinara wa kuasisti akifanya hivyo mara 15 na kufunga mabao saba.
Kuhusu mipango yake ndani ya Simba, Chama aliweka wazi kwamba bado ataitumikia Simba, ila kama ikitokea la kutokea hata yeye anaweza kusepa.
Mzambia huyo alisema kama Luis ataondoka basi naye kuna uwezekano wa kuondoka kama ikija ofa nzuri na uongozi wa Simba wakaikubali hali inayoleta sintofahamu ya hatima yake.
"Ndani ya miaka mitatu nikiwa Simba, nimeshafanya mambo mazuri ya kutosha, hivyo kama ikija ofa na Simba wakaikubali basi naweza kuondoka" amesema Chama.


IMEANDIKWA NA DAUDI ELIBAHATI