Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

CAF yailima faini Mazembe, Supersport

Muktasari:

  • Shirikisho la Soka Afrika limekuwa mstari wa mbele kupiga vitendo vya vurugu viwanjani

 Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF” imezipiga faini TP Mazembe na Supersport United kwa kitendo cha mashabiki wao kuvamia uwanja wakati wa mchezo wa fainali ya pili iliyopigwa Novemba 25, 2017 kwenye Uwanja wa Lucas Moripe, Pretoria.

Kwa mujibu wa kanuni 83 na 151 ya adhabu, Supersport imetozwa faini ya dola 15,000 kwa kushindwa kuwa na ulinzi mzuri kwenye uwanjani.

Klabu hiyo ya Afrika Kusini pia imepewa onyo kwa tukio hilo kujirudia, hivyo kuna uwezekano wa kupewa adhabu ya kucheza mechi bila ya mashabiki.

Kwa upande wa TP Mazembe, wenyewe imepewa adhabu ya faini ya dola 5,000 kwa tabia za mashabiki wake kwa mujibu wa kanuni 82 na 83 ya nidhamu ya CAF.

Mazembe imefanikiwa kutetea ubingwa wake kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1 baada ya kulazimisha suluhu na Supersport katika mchezo wa pili.