Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Saido apangua kikosi yanga, Yacouba agoma

YANGA imetua jijini Arusha jana mchana tayari kwa mchezo dhidi ya Dodoma FC kesho. Kwa mara ya kwanza mshambuliaji wao mpya Said Ntibazonkiza ‘Saido’ ataanza kukipiga kwenye Ligi Kuu Bara.Ntibazonkiza alicheza mechi ya kwanza ya kirafiki dhidi ya Singida na kutupia mabao mawili.Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya Yanga, Hersi Said ameliambia Mwanaspoti kwamba Saido kila kitu kimekamilika imebaki kwa kocha tu uwanjani.“Kila kitu kimeshakamilika usajili wake mpaka vibali vyake vimeshakamilishwa, sasa hakuna kitu kitazuia kucheza kwake, ni uamuzi wa benchi la ufundi kuona wanataka kumtumia vipi katika kikosi chetu,” alisema Hersi aliyesimamia usajili wa mshambuliaji huyo pendekezo la Kocha Cedrick Kaze.“Tulimuita mapema hapa nchini ili kila kitu kiweze kukamilika kwa haraka na hilo tumefanikisha, kila mmoja ana furaha kusikia hilo kwa sisi huku ndani ya uongozi na nafikiri mashabiki watakaokuja uwanjani pia watafurahia zaidi watakapomuona uwanjani.”Hersi aliongeza kuwa ameongea na Kaze na kumthibitishia kwamba Saido atacheza. “Wakati kocha tunamjulisha juu ya kukamilika kwa taratibu zote amefurahia hilo na ametuambia Saido kwa hatua hiyo atakuwa sehemu ya kikosi katika mchezo wa Jumamosi pale Arusha,” alisema Hersi. JEZI NAMBA 60Wakati Saido anatua nchini aliiambia Mwanaspoti kuwa ameomba kupatiwa jezi namba 10 lakini anayetumia kwa sasa Yacouba Sogne amegoma kumuachia.

Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh ameliambia Mwanaspoti kwamba mapema walisikia maombi hayo ya Saido na kuyafikisha kwa Yacouba lakini akagoma.“Yacouba alisema hata yeye anataka kutumia jezi hiyo jambo zuri hata Saido mwenyewe aliongea na Yacouba nafikiri walielewana, kwa hiyo Yacouba ataendelea kutumia jezi hiyohiyo.“Tumempatia Saido jezi namba 60 ambayo ameichagua mwenyewe,” alisema.