Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wawakikishi wetu CAF malizeni kazi nyumbani

WAWAKILISHI Pict

Muktasari:

  • Timu sita zinabeba bendera ya taifa letu katika anga la kimataifa: Simba, Yanga, Azam, Singida Big Stars, Mlandege na KMKM. Kila moja imetoka na matokeo tofauti katika mechi za kwanza ugenini na sasa zote zinahitaji nidhamu, mbinu na ari ili kufanikisha ndoto ya kusonga mbele.

WIKIENDI hii mashabiki wa soka la Tanzania Bara na Zanzibar wanatarajia kwa hamu kuona klabu zao zikikamilisha kazi katika mechi za marudiano za mashindano ya CAF.

Timu sita zinabeba bendera ya taifa letu katika anga la kimataifa: Simba, Yanga, Azam, Singida Big Stars, Mlandege na KMKM. Kila moja imetoka na matokeo tofauti katika mechi za kwanza ugenini na sasa zote zinahitaji nidhamu, mbinu na ari ili kufanikisha ndoto ya kusonga mbele.

Yanga ilipata ushindi wa mabao 3-0 ugenini dhidi ya Wiliete ya Angola, jambo linaloweka msingi mzuri wa kufuzu. Hata hivyo, wachezaji hawapaswi kuingia uwanjani kwa mtazamo wa sherehe mapema.

Ni lazima wajue mechi haijaisha hadi iishe na kutinga raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Inapaswa icheze kwa nidhamu ile ile waliyotumia ugenini. Safu ya ulinzi inapaswa kubaki makini, huku washambuliaji wakionyesha njaa ya kuongeza mabao.

PRE 01

Mechi ya marudiano inapaswa kutumika kuimarisha morali na heshima ya klabu, si kupunguza kasi kwa kudhani kazi imekwisha.

Hali kama hiyo pia inapaswa kwa Simba iliyoshinda kwa bao 1-0 ugenini, jiji Francistown, Botswana dhidi ya Gaborone United, ambapo licha ya  matokeo mazuri lakini yenye hatari.

Hali hii inahitaji Simba kuingia Kwa Mkapa kwa mechi hiyo ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa kwa kasi na shauku ya kufunga mapema. Bao la mapema litawapa amani na kuwafanya wapinzani watetereke. Kitu muhimu, Simba inapaswa kujiepusha na makosa madogo ambayo yanaweza kuwapa wapinzani nafasi ya kupata goli la ugenini.

Nidhamu, ubunifu wa washambuliaji na umakini wa mabeki vitakuwa msingi wa safari yao, ikizingatiwa Simba ina rekodi ya kuwahi kutolewa katika michuano hiyo ikiwa nyumbani ikiwamoa ile na UD Songo ya Msumbiji na Jwaneng Galaxy ya Bostwana.

PRE 02

Kwa upande wa Azam FC iliyopo Kombe la Shirikisho Afrika ilishinda mabao 2-0 ugenini dhidi ya Al Merreikh Bentiu ya Sudan ya Kusini. Kwa Azam mechi hiyo ya marudiano nyumbani yanapaswa kuwa jukwaa la kuthibitisha ubora wao. Licha ya ushindi huo mzuri ugenini, bado Azam haipaswi kujiamini kupita kiasi. Ishuke Azam Complex, ikitafuta bao moja la mapema na kudhibiti kasi ya mechi na bao hilo litakuwa limeiweka katika nafasi salama ya kusonga mbele.

Ni muhimu pia kuhakikisha safu ya ulinzi inabaki thabiti ili kuepuka presha zisizo za lazima iwapo wapinzani watapata bao.

Singida Black Stars wawakilishi wengine wa  Tanzania katika Kombe la Shirikisho Afrika iliipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Rayon Sports ugenini.

PRE 03

Huu ni ushindi wa thamani kubwa, lakini tofauti ni ndogo. Mwanaspoti linadhani ni vyema Singida kutokuridhika na bao moja pekee. Inapaswa kushambulia kwa kasi nyumbani, ikitafuta angalau goli la mapema litakalowavunja nguvu Wanyarwanda. Nidhamu ya kiakili na umakini wa wachezaji wa mstari wa mbele vitakuwa ufunguo wa Singida kuandika historia mpya.

Kwa wawakilishi kutika Zanzibar, KMKM iliyopo Kombe la Shirikisho iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ugenini dhidi ya AS Port ya Djibouti. Ni matokeo mazuri, hasa kwa kuwa ilifunga ugenini, licha ya kuwa ulichezwa New Amaan, Zanzibar na mechi ya marudiano inayopigwa uwanja huo huo leo Ijumaa ni nafasi yao ya kuvuka raundi ya kwanza kwa kulinda ushindi huo.

Hata hivyo, kupokea bao la wageni kunapaswa kuwa somo kwa kurejea bao la ugenini lina maana kubwa kwa soka la Afrika. Hivyo  KMKM inapaswa kujilinda kwa umakini huku ikitafuta mabao ya kutosha nyumbani. Bao moja tu litatosha kuiweka katika hali ya utulivu, lakini itapaswa kuhakikisha wageni hawapati nafasi ya kuamsha matumaini kwa kufunga bao lolote.

PRE 04

Wawakikishi pekee wa Tanzania iliyopoteza mechi zilizopita, Mlandege bado ina nafasi ya kusahihisha makosa kwa kupindua meza dhidi ya Insurance ya Ethiopia kwa kutumia vyema uwanja wa nyumbani kulipa kisasi cha mabao 2-0 iliyopewa ugenini. Mwanaspoti inaamini mechi ya marudiano nyumbani ni fursa ya kufa au kupona kwa mabingwa hao wa visiwani. Kitu muhimu kwao ni kuingia na kasi ya kushambulia tangu dakika za mwanzo, wakitafuta bao litakalowasha moto wa imani. Hii ni mechi ya nidhamu na ujasiri; Mlandege inapaswa kucheza bila hofu, kwa sababu hawana cha kupoteza.

Kwa jumla, nafasi ya klabu za Tanzania kusonga mbele ni kubwa zaidi kuliko misimu mingi iliyopita. Ikiwa na maana ushindi wa ugenini wa Simba, Yanga, Azam, Singida na KMKM ni ishara kwamba timu zetu sasa zinajiona washindani barani Afrika na si watalii. Changamoto kubwa ipo katika mechi hizo za  marudiano: nidhamu, umakini na kutokuridhika na matokeo ya awali inaweza kuwabeba. Hii ndio nafasi ya kuonyesha dunia kwamba soka la Tanzania linapiga hatua. Mwanaspoti linazitakia kila la kheri timu zote.