Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Wasanii wana cha kujifunza kwa Lady Jay dee

Muktasari:

  • Lady Jaydee, mwenye miaka 47, ni mfano wa wasanii ambao kizazi cha zamani na hiki cha sasa kinaweza kujifunza kitu kwao.

KUNA mastaa wa muziki wanaokuja na kuondoka kama upepo, lakini kuna wengine muda unapita na wao bado wanasikika, wanaheshimika na kazi zao zinaendelea kuwa sehemu ya historia.

Lady Jaydee, mwenye miaka 47, ni mfano wa wasanii ambao kizazi cha zamani na hiki cha sasa kinaweza kujifunza kitu kwao.

Judith Wambura maarufu Lady Jaydee a.k.a Komando Jide alianza safari yake rasmi ya muziki mwaka 2000, akaja na albamu yake ya kwanza, Machozi, na ndani ya miaka hiyo 26 amepita kwenye misukosuko, mabadiliko ya muziki, ushindani na vizazi vipya bila kupoteza jina lake.

Leo hii, wakati mastaa wengi wanakimbizana na umaarufu wa muda mfupi, Lady Jaydee anaendelea kuwa somo la uvumilivu, nidhamu, ubunifu na namna ya kujenga kazi inayoweza kudumu. Kuna mambo mengi mazuri ambayo mastaa wa sasa wanapaswa kujifunza kutoka kwake.


ELIMU HAISHI

kabla hajawa Lady Jaydee wa leo,alisomea Uandishi wa Habari TIME School of Journalism (TSJ), Dar es Salaam, ngazi ya Astashahada, na kufanya kazi kwa muda mfupi Clouds FM.

Sambamba na safari yake ya muziki, alishiriki na kushinda shindano la kuimba katika kipindi cha DJ Show cha Radio One, ushindi uliomfungulia nafasi ya kurekodi katika Studio za MJ Records.

Kutoka hapo, aliendelea kujijenga kwenye muziki hadi kuwa miongoni mwa wasanii walioweka alama kubwa katika Bongo Fleva.

Sasa ameongeza ukurasa mwingine wa uandishi wa kitabu chake alichokizindua Juni 2025 kiitwacho Diary ya Lady Jaydee, akieleza alitaka simulizi ya maisha yake na yasikike moja kwa moja kutoka kwake, bila kupita kwa watu na kubadilishwa njiani.


MGUSO WAKE KWA MASTAA

Jide hakujenga safari yake kwa kuona kila msanii ni mpinzani, amekuwa na kolabo na mastaa mbalimbali. Miongoni mwa matukio ya hivi karibuni yaliyovuta hisia kubwa za mashabiki ni lile la Septemba 17, 2026.

Mkongwe huyo alimzawadia Diamond Platnumz kitabu chake Diary ya Lady Jaydee, baada ya kukutana naye kwenye chakula cha jioni. Tukio hilo liliongeza pia shauku ya mashabiki wanaotamani siku moja kuwaona wa wili hao wakifanya kolabo.

Lakini si hivyo tu, Jide am ekuwa msanii ambaye huwezi kumsikia kama anabifu la aina yoyote na msanii wa kizazi kipya au hata wale wa enzi zake, zaidi utamuona akiungana nao kwenye matukio maalum.


HANA MPINZANI

Licha ya kufanya mziki kwa miaka mingi lakini hakuna msanii ambaye amewahi kufikia ladha ya sauti ya Jide, hilo linaweza kuwa jambo linalomfanya awe wa tofauti na kujizolea mashabaki wenye kiu ya kusikia ngoma zake.

Kumekuwa na wasanii wengi wakike ambao wanafanya vizuri lakini hakuna hata mmoja ambaye unaweza kumfananisha na mkongwe huyo, ukiachilia mbali nyimbo zake ambazo zinaishi miaka yote.

Jide amekuwa na nguvu ya kukaa miaka hata mitatu bila kutoa ngoma hata moja na siku atakayotoa basi utaisikia kila mahali tena ikiwa na utofauti mkubwa kuliko zile unazosikiliza kila siku.

Licha ya miaka mingi aliyodumu kwenye Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva, Lady Jaydee bado ana kijji kikubwa cha mashabiki wa kizazi na kizazi.

MTU WA WATU

Maisha ya nje ya muziki, Jide anaonekana mara nyingi na watangazaji maarufu Edo Kumwembe, Oscar Oscar na Shaffih Dauda ni miongoni mwa watu ambao wamekuwa karibu naye nje na maswala ya muziki.

Hii inaonyesha wazi Jide anawatu wengi nje na mashabiki wa muziki wake na wasanii wenzake ambao wanafanya kazi moja.


MITANDAONI BADO ANABAMBA

Teknolojia haijamwacha nyuma Jide, badala yake anaenda nayo sambamba, akitumia majukwaa ya kidijitali kuendelea kuwafikia mashabiki zake kwa ukubwa zaidi.

Kwa sasa kwenye mtandao wa YouTube amefikia views milioni 38.6, huku wimbo wake wa “Mambo Matano” ukishafikisha zaidi ya views milioni 3.6, “Siku Hazigandi” milioni 2.6 na “I Found Love” zaidi ya milioni 1.3.

Hata Bwana Angu, iliyotoka mwaka 2025, imevuka views 894,000, ikionyesha kuwa hata baada ya miaka mingi kwenye muziki, Jide bado ana nafasi kwenye masikio na macho ya kizazi cha sasa.


ANALINDA CHAPA YAKE

Miaka imepita lakini Jide bado amebaki na mwonekano wake uleule unaomtambulisha siku zote hajawa mtu wa kubadilika kila linapokuja suala la mtindo mpya amekuwa akijiweka vizuri na kutunza muonekano wake kwa namna ambayo inamfanya aendelee kuo nekana wa wakati wote.

Ni aina ya msanii ambaye kadiri miaka inavyosogea, ndivyo anavyozidi kuujua umuhimu wa kujitunza na kuilinda taswira yake mbele ya mashabiki, licha ya umri wake mkubwa ila ukimuona na kama binti wa miaka 25.

MAISHA YAKE NI SIRI YAKE

Jide pia amejua kutenganisha umaarufu na maisha binafsi, hasa suala la mahusiano, si mtu wa kuweka kila jambo mitandaoni. Hilo ni somo kwa mastaa wanaoamini kila kinachotokea lazima kifike Instagram.


SAUTI, SHOO NA HESHIMA

Sauti yake ndiyo moja ya silaha kubwa iliyombakiza kwenye muziki, ni zaidi ya miaka 25 bado anaimba kwa utambulisho uleule, huku shows zake zikiwa na hadhi ya kipekee.

Mwaka 2025, Silver Concert ilikuwa na tiketi za kuanzia Sh 50,000, huku VIP/VVIP zikiwa juu zaidi na zote zilimalizika kabla ya siku ya tukio, hii ni ishara ya namna jina lake linavyoweza kuvuta mashabiki kwenye maonyesho makubwa.

Uhusiano wake na mashabiki ni kitu kingine kwani miaka inapita lakini bado watu wanataka kumuona jukwaani.

Silver Concert ya 2025 iliyoadhimisha miaka 25 ya muziki wake ilijaza ukumbi wa Superdome na kuwakutanisha mastaa wa vizazi mbalimbali.

NYIMBO MPYA, MAPOKEZI YAKE

Jide hajakaa kwenye mafanikio ya zamani kwani Silver ya 2025 ilikuwa na nyimbo 25, zikiwamo Po Po, Bwana Angu, Mambo Matano, Marafiki akiwa na Fid Q na Po Po Remix akiwa na Rapcha, Frida Amani na Wakazi. Hapo ndipo somo la Jide linapokamilika, jenga muziki, jenga watu, linda maisha yako, kubali mabadiliko na usiache kutoa kazi mpya. Miaka inaweza kwenda, lakini ukijua kuitunza kazi yako, jina lako linaweza kubaki.