Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NIKOLA JOKIC... MVP anayetamba na pesa zake NBA

Muktasari:

  • Lakini huyu ndio Lionel Messi na Ronaldo wa kikapu kule Serbia, na bado anasumbua sana ndani ya NBA licha ya msimu huu kukosa mechi kadhaa kutokana na matatizo ya kifamilia.

DENVER, MAREKANI: HADI sasa Nikola Jokic ndio anashikilia rekodi ya kuwa MVP wa Ligi Kuu ya Kikapu ya NBA aliyeshinda tuzo hiyo akiwa na wastani wa chini ya pointi 25 kwa mechi moja.

Lakini huyu ndio Lionel Messi na Ronaldo wa kikapu kule Serbia, na bado anasumbua sana ndani ya NBA licha ya msimu huu kukosa mechi kadhaa kutokana na matatizo ya kifamilia.

Staa huyu anayeichezea Denver Nuggets ameshinda tuzo ya MVP mara tatu, awamu mbili ikiwa ni mfululizo msimu wa 2020-21 na 2021-22.

Mwaka huu  alikuwa MVP wa msimu wa kawaida, lakini bado yupo katika orodha ya mastaa wanaopewa nafasi ya kushinda tuzo hiyo mwisho wa msimu huu.

Ukiondoa mafanikio aliyopata ndani ya uwanja hadi kufikia kupata tuzo hizo na kushinda taji la NBA mwaka 2023, staa huyu mfukoni pia yuko sawa, ana utajiri wa kutosha.

ANAPIGAJE PESA

Anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 80 milioni. Chanzo chake kikubwa cha mapato ni kupitia mshahara anaoukunja katika timu yake ya Denver Nuggets.

Juni, 2022, Nikola alisaini mkataba mnono wa miaka mitano wenye thamani ya Dola 264 milioni uliomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi kwa wakati huo.

Kwa mujibu wa vipengele vilivyowekwa, katika msimu wake wa kwanza wa 2022/23 Jokic alipata Dola 32 milioni kisha itakaongozeka na msimu wa mwisho ambao ni 2027/28 atapata Dola 60 milioni,

Kabla ya mkataba huo, aliwahi kuongeza mkataba mwaka 2018 ambapo alisaini dili la miaka mitano lenye thamani ya Dola 148 milioni.

Katika mikataba hiyo miwili tu, staa huyu anavuna Dola 412 kiujumla kupitia mshahara tu.

Mbali ya mshahara, staa huyu anapata mkwanja wa kutosha kutokana na madili mengine ya nje ya uwanja ambako amesaini mikataba ya udhamini na kampuni mbalimbali kama 361 Degrees, Western Union,  Somborac na Panini ambayo kwa mwaka anaingiza Dola 8 milioni, kwa mujibu wa Forbes.

Pia amewekeza huko Serbia ambako amenunua nyumba mbalimbali katika eneo la Sombor na anataka kujenga viwanja vya kuchezea mpira wa kikapu.

Kwa sasa ni mmiliki mwenza wa timu ya mpira wa kikapu,  BC Mega Basket, ambayo aliwahi kucheza hapo awali kabla hajatua NBA.


MJENGO

Nikola anamiliki nyumba yenye thamani ya Dola 2.4 milioni huko Denver, Colorado aliyoinunua mwaka 2019, ndani yake ina vyumba sita vya kulala na vyoo saba pia ina bwawa la kuogelea na sehemu ya kufunyia mazoezi yake binafsi.

NDINGA ZAKE

GMC Denali-Dola 65,000

 Lamborghini Aventador S-417,000

 2021 Mercedes-Benz AMG G 63 Brabus-536,122

Lamborghini Urus-221,506

 Porsche-Mansory Panamera 4S-110,900


MSAADA KWA JAMII

Amekuwa akitoa sana misaada nchini Serbia hususani katika eneo la Sombor ambako amezaliwa na wakati wa mlipuko wa virusi vya Corona alijenga hadi hospitali katika eneo hilo.

Akiwa Marekani anatajwa kuwa ni mdau mkubwa wa taasisi ya LuBird’s Light Foundation ambayo amekuwa akiichangia pesa kutimiza majukumu mbalimbali ya kijamii.

BATA NA MAISHA BINAFSI

Yupo katika ndoa na mrembo Natalija Jokic ambaye alikuwa ni mchumba wake tangu wapo shuleni udogoni. Wawili hawa walifunga ndoa mwaka 2020 na hadi sasa wamebahatika kupata watoto wawili, wa kike aitwaye Ognjena na wakiume ambaye amezaliwa hivi karibuni na bado jina lake halijapatikana.