Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nidhamu mbovu zinagharimu timu zisitetewe

SOWAH Pict

Muktasari:

  • Imeshatembeza rungu la kifungo cha mechi tano kwa kila mmoja kwa wachezaji wanne tofauti ikiambatanisha na faini ya fedha Sh1 milioni juu kwa makosa ambayo wachezjai hao wameyafanya.

BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kupitia Kamati yake ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi, imekuwa na ukali sana kwa wachezaji watovu wa nidhamu uwanjani hasa wanaopiga wenzao.

Imeshatembeza rungu la kifungo cha mechi tano kwa kila mmoja kwa wachezaji wanne tofauti ikiambatanisha na faini ya fedha Sh1 milioni juu kwa makosa ambayo wachezjai hao wameyafanya.

Jambo zuri ambalo hapa kijiweni tunaona kama litakuwa la mfano ni kwamba wachezaji hao waliopewa adhabu ni wa timu kubwa nchini za Yanga, Simba na Singida Black Stars ambao ni Khalid Aucho, Allasane Kante, Jonathan Sowah na Ibrahim Abdullah ‘Bacca’.

Adhabu inayouma kama hiyo ya kufungiwa mechi tano na kutozwa faini ya fedha, itamfanya mchezaji abadilike baada ya kumaliza kuitumikia kwa sababu akirudia tena michezo isiyo ya kiungwana, maana yake atakaa nje tena kwa muda mrefu na atarudia kutoa fedha za faini.

Na hii haitoishia kwa mchezaji au wachezaji tu bali pia hata timu itapata fundisho baada ya adhabu kama hizo jambo ambalo linaweza kuifanya izidi kusimamia nidhamu na maadili kwa wachezaji wake ili wasiwe wanakutana na adhabu kama hiyo.

Iko wazi kwamba mchezaji anapofungiwa, timu yake nayo inaathirika kwa kiasi kikubwa na baadhi ya hasara hizo kwa timu ni kupungua kwa nguvu ya kikosi ikiwa mchezaji aliyefungiwa ni muhimu, kusababisha timu kupoteza mechi au kushindwa kufikia malengo ya ushindi.

Fikiria timu inamkosa mchezaji katika michezo mitano ya ligi kisa tu alimpiga mwenzake, jambo ambalo kwanza sio la kiungwana, lakini pia halina sababu ya msingi.

Inaweza kueleweka kama mchezaji anakosa mechi kwa adhabu itokanayo na rafu ya kawaida ya kimchezo kuliko kumpiga au kufanya kitendo cha kudhalilisha mwingine.

Wachezaji wa timu zetu wanatakiwa kutuachia sisi huo usela wao na kisha wenyewe wakajikita na kazi yao ambayo ni kucheza soka.