Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Inspector Haroun afunga mwaka na ngoma mbili

INSPEKTA

Muktasari:

  • Kwa upande wa  mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Haroun Rashid Kahena a.k.a Inspekta Haroun au Babu, ameamua  kufunga mwaka kwa kuachia ngona mbili ambazo ni 'AI' (Akili mnemba) na 'Maisha Ndio Haya Haya'.

MWAKA 2025 ukiwa unaelekea ukingoni, wasanii baadhi wameachia ngoma ambazo zimekuwa kama ni funga mwaka kwa upande wao na mashabiki.

Kwa upande wa  mkongwe wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Haroun Rashid Kahena a.k.a Inspekta Haroun au Babu, ameamua  kufunga mwaka kwa kuachia ngona mbili ambazo ni 'AI' (Akili mnemba) na 'Maisha Ndio Haya Haya'.

Inspector Haroun ambaye aliwahi kutamba na nyimbo kama, Asali Wangu wa Moyo na Mtoto wa Get Kali, amesema, lengo la kutoa nyimbo mbili kwa pamoja ni kwa ajili ya kuwapa zawadi mashabiki zake ambao kwa wale wa Hip Hop watafurahi na wimbo wa 'AI' (Akili Mnemba) na wale mashabiki wa Amapiano watafurahishwa na wimbo wa 'Maisha ndio Haya Haya'.

INSP 01

"Lengo la kuachia nyimbo hizi mbili ni kwa ajili ya kuwapa zawadi mashabiki zangu, na ndio maana zipo kwenye mahadhi tofauti, moja AI ni mahadhi ya Hip-hop, Maisha Ndio Haya Haya ina mahadhi ya Amapiano 

"Hivyo na imani mashabiki zangu watafurahishwa na hii zawadi, sababu kwa mwaka huu mwezi wa saba nilitoa wimbo wa Final Sub niliomshirikisha Ibraah, ambao mahadhi yake ni Hip-hop, sasa ukiangalia hadi sasa imepita miezi mitano bila kutoa nyimbo, ndio maana nasema hii ni zawadi kwa mashabiki zangu," amesema Inspector Haroun.

INSP 02

Mbali na hayo, Inspector Haroun, amesema: "Mimi sina tatizo na wananchi, naishi nao vizuri, sijawahi kupata kadhia yeyote kutoka kwa Gen-Z, niseme tu mimi nina rasilimali watu, naamini kazi zangu zitaenda vizuri tu huko kwenye mitandao ya kijamii nilipoziachia."