HARMONIZE, KAJALA: Wamefunga 2025 kama walivyoanza 2016
Muktasari:
- Wawili hao unaweza kusema walivyoufungua mwaka 2021 kwa kuanika rasmi uhusiano wao kwa mara ya kwanza katika Sikukuu ya Wapendanao Februari 14, 2021, ndivyo walivyoufunga mwaka huu wa 2025 katika Sikukuu ya Krismasi kwa kuweka wazi kuwa wamerudiana.
MASTAA wawili, Harmonize na Kajala Masanja walianza kama utani na kuuweka hadharani uhusiano wao 2021 huku watu wengi wakidhani kwamba ilikuwa ni kiki.
Wawili hao unaweza kusema walivyoufungua mwaka 2021 kwa kuanika rasmi uhusiano wao kwa mara ya kwanza katika Sikukuu ya Wapendanao Februari 14, 2021, ndivyo walivyoufunga mwaka huu wa 2025 katika Sikukuu ya Krismasi kwa kuweka wazi kuwa wamerudiana.
Baada ya Kajala kuvishwa pete Desemba 29, 2025 kuvishwa pete Kajala, tukio hilo limezua gumzo huko kwenye mitandao ya kijamii, watu wanamsema Kajala kuwa amelamba matapishi ambayo aliapa hawezi kuyarudia tena.
Kajala amezungumza na Mwanaspoti kuhusu kauli yake ya kutorudiana na Harmonize, na pia kushambuliwa kwenye mitandao ya kijamii na watu kwa kuonekana kigeugeu.
Kajala amebainisha kwamba alikubali kurudaina na Harmonize kwa kuwa bado alikuwa anampenda, hivyo watu wamuache kwani maneno yake sio sheria wala Biblia.
Hata hivyo, alisema kuwa tayari alikuwa amesonga mbele na maisha yake, baada ya kuachana na Harmonize, lakini kama wameyazungumza na kuombana msamaha na bado kila mmoja anampenda mwenzake kwanini wasirudiane?
"Watu wanisamehe tu maana siwezi ficha hisia zangu kwa mtu ninayempenda, nimerudiana na Harmonize kwa sababu nampenda. Japo Nili-move on, lakini ilikuwa mtu ambaye bado yupo. Alafu tumezungumza na kumaliza tofauti zetu ,tumeombana msamaha kwanini tusirudiane? watu inabidi waelewe tu, hivyo haraka wakinitukana au kunisema sidhani kama nitawaelewa, sababu nishafanya uamuzi, cha kufanya waachane na yaliyopita, wagange na haya ya sasa hivi," anasema Kajala.
Kajala amevishwa Pete na msanii wa Bongofleva, Harmonize, ikiwa ni pete yake ya pili, baada ya kuachana kwa muda wa mwaka mmoja 2024 kwa madai ya Kajala kuwa Harmonize alikuwa anamchukulia poa kwa kila kitu sababu ya mazoea kitu ambacho alipitiliza na kukerwa nacho.
Lakini kabla ya mwaka huo 2024, Kajala alitokea kumtema Harmonize Aprili 2021 baada ya kumkuta akimtongoza bintie, Paula, ambaye kwa wakati huo alikuwa katika uhusiano na msanii Rayvanny.
Kajala alikuja kumsamehe Harmonize na alivishwa pete hiyo katika hafla iliyofana iliyoandaliwa jijini Dar es Salaam ilikuwa Ijumaa, Juni 2024.
Kitendo hiki kiliwashangaza watu wengi, kuwa Kajala kukubali kurudiana na Harmonize na hali ya kuwa amefanya kosa kwa mtoto wake kumtaka kimapenzi. Sio tu watu kushangazwa, hii hadi mtoto wake, Paula, hakupendezwa na tukio hili na aliandika kwenye akaunti yake ya Instagram kuwa bora afe kuliko kumuita Harmonize, baba. Akaweka picha ya utotoni mwake ambayo alipiga akiwa na wazazi wake prodyuza P-Funk Majani na Kajala.
Mrejesho wa uhusiano huo, haukudumu sana, kwani Harmonize na Kajala waliachana tena. Hapa ndipo Kalaja alipotamka kuwa hawezi kulamba matapishi tena kwa kumrudia Harmonize.
Kajala aliendelea kusema hadharani kuwa kurudiana na Harmonize baada ya staa huyo kumtaka kimapenzi Paula, ni sawa na kujali mapenzi kuliko bintiye huyo. Na aliamua kuachana naye kwa sababu alikuwa anachukuliwa kimazoea sana na Harmonize, ambaye alimtuhumu muimbaji huyo kutokuwa tayari kutulia kwenye mapenzi.
"Naona kabisa nilikosea kipindi niliporudiana na Harmonize, kuna kipindi nilianza kujali mapenzi zaidi kuliko mtoto wangu wakati mtoto wangu ndiye anayenifahamu vizuri kuliko mtu mwingine yeyote. Niliona labda vitu ninavyovifanya mwanangu anajisikia vibaya na hana cha kufanya, ila kwa sasa nimejifunza nimeona wapi nilikosea na kuamua kurekebisha na siwezi kurudi nyuma ama kurudiana tena na huyo mwanaume," aliongeza Kajala wakati huo.
Hapa chini tukumbushane penzi lilivyokuwa na hekaheka ya kurudiana na kuachana.
2021 waliachana na kurudiana
Harmonize alimuomba msamaha Kajala kwa kosa la kumshawishi binti yake Paula wakati walipokuwa katika uhusiano, hivyo arejeshwe kwenye uhusiano. Kajala akamsamehe ila uhusiano huo ulidumu kwa miezi miwili mwaka 2021.
2022 kuachana mara ya pili
Ijumaa, Desemba 9, 2022, Kajala alitangaza kuwa wamemwagana tena na Konde Boy kwa mara ya pili.
2024 Kajala avishwa pete
Harmonize alimvisha pete mwigizaji Kajala katika hafla iliyofana iliyoandaliwa jijini Dar es Salaam Ijumaa ya Juni 24, 2024 na kuhudhuriwa na familia, marafiki wa watu wengine mashuhuri walioalikwa.
(WALIACHANA LINI BAADA YA PETE YA KWANZA?????????)
Machi 2025 tetesi za kurudiana
Tetesi za kurudiana kwa mastaa hawa wawili Harmonize na Kajala, zilianza Machi 27, 2025, baada ya kusambaa kwa video yao ikionyesha wakikumbatia katika mashindano ya soka ya Samia Cup. Tetesi hizo zilidai kuwa wamerudiana kisirisiri kwani Kajala anafanya kwa kujificha sababu hapendi kumkera mtoto wake, Paula, ambaye alikuwa hataki kusikia kuhusu uhusiano huo kurudi.
Mwanaspoti lilipiga stori na wawili hao Harmonize na Kajala kwa nyakati tofauti, Kila mmoja alikana kutokuwepo na mahusiano zaidi ya kumaliza tu tofauti zao na kuishi kama marafiki.
Mei 2025 Harmonize ndani birthday party ya mtoto wa Paula na Marioo
Tetesi za kurudiana kwa Harmonize na Kajala ziliendelea, baada ya Harmonize kufika katika sherehe ya kuzaliwa mtoto wa msanii wa Bongofleva Marioo na Paula iliyofanyika jijini Dar es Salaam, huku Kajala kuonyesha mahaba kwa Harmonize, hapo walizidi kuwaacha watu wengi njiapanda kwa kutokujua kama wamerudiana au laa! Maana muda wote walionekana wakiwa katika mahaba mazito.
Mwanaspoti lililokuwa katika sherehe hiyo, lilibahatika kuongea na wawili hao kwa nyakati tofauti kujua undani wa suala hilo tena na kila mmoja alikanusha kurudiana.
Mashabiki nao walipamba moto na kudai kuwa, hata mwanzo walivyokuwa wapenzi kisha wakaja kuachana, kabla ya kurudiana walianza kwa kuonekana hivi hivi kupitia mitandao wakiwa pamoja na baadaye wakaweka wazi kuwa wamerudiana.
Des 29, 2025 pete ya pili
Baada ya kukanusha kanusha miezi saba iliyopita kuwa hawajarudiana, sasa Desemba 29 2025, mwanamuziki Harmonize alimvisha pete ya uchumba Kajala. Lakini kabla ya hiyo Pete siku ya Sikukuu ya Krismasi Desemba 25, 2025 kwenye show ya Harmonize iliyofanyika Visiwani Zanzibar, walionekana Harmonize na Kajala wakiwa pamoja, na kwenye shoo hiyo Harmonize alimpandisha Kajala kwenye jukwaa kusalimia. Hapa ndio watu wakaanza kuamini wamerudiana na wapo waliosema ni kiki ya kuipeleka mjini wimbo wake mpya wa alishirikiana na Mbosso kuimba.
Kwenye hilo tukio sasa la kuvalishana pete, ambalo ilifanyika katikati ya bahari kwenye yatch, Harmonize ameeleza vitu ambavyo amekuwa akivikumbuka kutoka kwa Kajala baada ya kuachana naye ni kuwa ni ukaribu wake pamoja na sapoti aliyokuwa akimuonyesha.
"Nilimisi vitu vingi, lakini cha umuhimu zaidi ni utu wake, utu wake unanifanya nakuwa 'serious', utu wake unanifanya nakuwa 'hard worker', unanipa utulivu, utu wake unanipa utulivu wa kufikiria maisha, kingine ameifanya my house kuwa home, akiwa nyumbani kwangu yaani kunageuka kuwa nyumbani nikisema hivi nadhani kila mtu ananielewa," amesema Harmonize.
Mipango ya ndoa na hashtag yao ni #HK4ever. Wakati tukio hilo likiendelea wawili hao walitangaza kuwa watafunga ndoa 2026 huku hashtag yao rasmi ikiwa ni #HK4ever.