Yanga yakaa mezani na meneja wa kipa Kakolanya
Muktasari:
Meneja huyo amefikia hatua hiyo baada ya kueleza kwamba Kakolanya anahitajika kuongezewa thamani na akihoji kwa nini hapewi nafasi.
Baada ya Meneja Seleman Haroub wa mchezaji Beno Kakolanya kutaka kupeleka barua Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) , uongozi wa klabu ya Yanga umeamua kukaa chini na meneja huyo ili kuzungumza kwa mara ya mwisho juu ya hatima ya mchezaji huyo ndani ya kikosi hicho.
Akizungumza na MCL Digital, Meneja huyo alisema ameketi chini na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo na kuzungumza upya, wamekubaliana baadhi ya vitu.
“Sisi sote ni binadamu hivyo tuliwasiliana na uongozi husika na kukubaliana upya baadhi ya vitu, kwahiyo mazungumzo yetu yalikuwa mazuri ndio maana sikufika mbele zaidi nikaona ngoja tusubilie makubaliano yetu kama yataenda kama tulivyopanga,” alisema.
Haroub aliongeza kwamba mchezaji wake anahitaji ili kuongeza thamani yake, hivyo kuwa katika malumbano ya kila mara na mwajiri wake huku ukiwa huchezi inakuwa haipendezi ndio maana wameona wakae chini upya baada ya uongozi kutaka hivyo.