Yanga, Simba wachapana makonde Uwanja wa Uhuru
Dar es Salaam. Makonde yamerushwa na walinzi wa timu za Simba na Yanga maarufu kama Makomandoo wakati klabu hizo mbili zilipokuwa zinaingia uwanjani kabla ya pambano lao kuanzia kwenye uwanja wa Uhuru, saa 10.00 jioni.
Timu hizo mbili ziliingia uwanjani hapo kuanzia saa 8.00 mchana ambapo Yanga walitangulia na robo saa baadaye Simba walifuatia.
Makondoo wa Yanga, walilizingira basi lao ili kuzuia wachezaji kuguswa na mtu yeyote na wakati Simba wanaingia, mmoja wa makomandoo hao alikwenda kumwaga maji mbele ya basi la Simba jambo lililowafanya wale wa Simba kuanzisha vurumai.
Zogo hilo lilimalizwa baada ya askari waliovaa kiraia, kwenda kumtoa komandoo wa Yanga aliyemwaga maji na kumweka mikononi mwao.