Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ujio wa Tambwe wabadili upepo

MKALI wa mabao wa Yanga, Amissi Tambwe, amerejea kwa kishindo klabuni hapo na anatarajiwa kupangua kikosi cha kwanza cha kocha George Lwandamina.

Tambwe tayari ameifungia timu hiyo mabao 46 ya Ligi Kuu Bara tangu alipojiunga nayo mwishoni mwa 2014. Nyota huyo raia wa Burundi yupo fiti baada ya kuwa nje ya Uwanja kwa kwa miezi miwili.

Kurejea kwa Tambwe aliyekuwa majeruhi, kunatarajiwa kuwatikisa washambuliaji wengine klabuni hapo akina Ibrahim Ajibu, Donald Ngoma na Obrey Chirwa ambapo mmoja atalazimika kumpisha katika kikosi cha kwanza.

Awali, Tambwe alifanya vizuri pindi akicheza sambamba na Ngoma ambapo msimu wa 2015/16 kwa pamoja walifunga mabao 38 ya ligi na kuwa pacha kali zaidi ya ushambuliaji katika kipindi cha zaidi ya muongo mmoja.

Hata hivyo uwepo wa Ajibu huenda ukapangua pacha hiyo kwa Lwandamina kumpanga na Tambwe ama kuwatumia watatu pamoja na Ngoma kwenye mchezo unaofuata dhidi ya Kagera Sugar.

Nyota wa zamani wa Yanga, Aaron Nyanda, amefichua kuwa Tambwe hana mpinzani katika kikosi cha kwanza na huenda kocha Lwandamina akalazimika kumpunguza kiungo mmoja ama mshambuliaji mmoja kumpisha.

“Tambwe lazima aanze na Ngoma (Donald) katika kikosi cha kwanza. Ajibu (Ibrahim) anaweza kuanza katika winga moja na kocha atabaki na maamuzi ya kuangalia nani kati ya Pius Buswita na Obrey Chirwa anastahili kuanza,” alisema Nyanda.

Yanga imekuwa na ukame wa mabao msimu huu na katika mechi tano za mwanzo imefunga manne tu, lakini Lwandamina anaamini  kurejea kwa Tambwe kunaweza kuongeza kasi yao ya ufungaji.

Nyota mwingine wa zamani wa Yanga, Ali Yusuph ‘Tigana’ alisema Tambwe na Ngoma walifanya vizuri pamoja, lakini sasa kocha Lwandamina anaweza kujaribu kombinesheni mpya ya Tambwe na Ajibu.

“Bado Ngoma hajawa vizuri sana tangu alipotoka benchi la majeruhi, nimemuona Ajibu yuko vizuri, pengine kocha anaweza kumjaribu na Tambwe,” alisema Tigana.