Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ubingwa Simba upo mikoani

SIMBA inausotea ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa tano sasa, lakini kama mabosi wa timu hiyo watapiga hesabu vema kwa mechi zao za mikoani na kushinda, basi ni wazi mashabiki wa klabu hiyo wajiandae tu kucheka msimu huu.

Hata beki kisiki wa Azam, Yakub Mohammed ameamua kuitaja Simba kuwa ni kati ya timu zinazowapa presha Azam katika mbio za ubingwa kutokana na kuonekana kuwa wazuri msimu huu kulinganisha na watetezi Yanga, lakini kiungo Mghana, James Kotei akafichua kitakachowapa Simba ubingwa msimu huu.

Kotei ameiangalia ligi ya safari hii na kubaini mechi za mikoani ni ngumu na kama klabu yoyote ikiwamo Simba itafanya vema katika mechi zao zilizobaki basi taji ni lazima kombe liende kwa mkali huyo.

Mghana huyo alisema mechi za ugenini msimu huu ndizo zitakazoamua bingwa kutokana na kuwa ngumu kuliko zile za nyumbani, lakini akaipa nafasi kubwa timu yake kufanya kweli kama itakomaa na mechi hizo ngumu za mikoani.

“Tumepata pointi nne ugenini, haikuwa jambo rahisi. Mechi za ugenini ni ngumu kutokana na safari kuwa ndefu, ila pia viwanja ni vigumu kucheza, lakini bado naamini tuna nafasi ya kurekebisha makosa ya msimu uliopita,” alisema.

Vinara hao wa Ligi Kuu Bara wamesaliwa na mechi 10 za mikoani ambazo kama wakishinda zote watapata jumla ya pointi 30, hizo ni mbali na michezo miwili watakayokuwa ugenini dhidi ya Yanga na Ruvu Shooting.

Simba ni moja ya timu zinazopewa nafasi kubwa ya kuwa bingwa msimu baada ya kuukosa kiduchu msimu uliopita walipozidiwa ujanja na watani zao Yanga na beki wa Azam, Yakub Mohammed ameitaja Simba kuwa ndio inayowanyima usingizi VPL.

Yakubu ambaye tangu ajiunge na Azam Desemba mwaka jana, ameichezea mechi 18 na ukuta wao kuruhusu mabao manne tu, alisema Simba ina wachezaji wa kiwango cha juu kuliko Yanga ambayo imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu kwa mara tatu mfulululizo.

“Naitazama Simba kama timu ambayo itatupa ushindani mkubwa zaidi. Ina kikosi chenye ubora zaidi ya Yanga,” alieleza beki huyo aliyechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Azam wa mwezi Agosti.

Aliongeza kusema: “Timu yetu ndiyo ina nafasi kubwa zaidi katika mbio za ubingwa msimu huu. Tuna kikosi kizuri na cha ushindani. Changamoto kubwa kwetu ni kuongeza idadi ya mabao tunayofunga. Bado kasi yetu sio nzuri sana katika eneo la mwisho.”

MECHI ZA UBINGWA

Baada ya Simba kucheza mechi mbili za mkoani dhidi ya Mbao na Stand United na kuvuna pointi nne, itakuwa na kibarua kwa mechi nyingine 10 ambazo kama itafanya kweli itaondoka na pointi zote 30.

Simba imekuwa na matokeo mazuri kwenye uwanja wa nyumbani mpaka sasa na msimu uliopita ilipata matokeo mazuri hata kwenye viwanja vigumu vya ugenini kitu kinachowapa jeuri mashabiki wao kuamini msimu huu watapeta.

Mechi hizo 10 za mkoani ni mbili za jijini Mbeya dhidi ya Mbeya City na Prisons, itaenda Mtwara kuifuata Ndanda, itaifuata Majimaji mjini Songea, kisha kurudia Shinyanga kuvaana na Mwadui pia itaenda Njombe na Iringa kucheza na Njombe Mji na Lipuli.

Nyingine ni dhidi ya Singida United mjini Singida, Kagera Sugar mjini Bukoba na ile ya Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar, huku Ruvu Shooting licha ya kuwa wenyeji, lakini italazimika kuifuata Simba Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Hata hivyo mechi zinazoweza kuitibulia Simba ni ile ya Namfua dhidi ya Singida, Kagera mjini Bukoba na pengine Mtibwa mjini Morogoro kwani timu hazitabiriki.