Simba yamkaba Tshishimbi mapemaa!

Muktasari:

Kotei ambaye ameanza katika mechi zote za Simba msimu huu, alikiri kuwa katika mechi ya Ngao ya Hisani, Tshishimbi ndiye aliyetibua mipango yao ya ushindi lakini amedai kuwa alikuwa bado hajakumbana na ugumu wa Ligi Kuu hivyo katika mechi ya Oktoba 28 hatakuwa moto tena.

KIUNGO wa Simba, James Kotei aitazama Yanga ambayo watakutana nayo wiki mbili zijazo na kudai kuwa kwa sasa wakimdhibiti vilivyo kiungo wao, Papy Kabamba Tshishimbi, mambo yatakuwa magumu kwa watani zao hao.
Kotei ambaye ameanza katika mechi zote za Simba msimu huu, alikiri kuwa katika mechi ya Ngao ya Hisani, Tshishimbi ndiye aliyetibua mipango yao ya ushindi lakini amedai kuwa alikuwa bado hajakumbana na ugumu wa Ligi Kuu hivyo katika mechi ya Oktoba 28 hatakuwa moto tena.
Kiungo huyo raia wa Ghana alifichua kuwa Yanga ya sasa inamtegemea sana Tshishimbi tofauti na msimu uliopita ambapo Haruna Niyonzima na Saimon Msuva ndiyo walikuwa tishio zaidi.
"Aling'ara katika mechi iliyopita kwa kuwa alikuwa ndiyo kwanza ameingia nchini, hakuwa amekutana na ugumu wa Ligi, pia tulimwacha sana acheze peke yake na ndiyo sababu alituvuruga," alisema Kotei.