Dortmund yamtia kifungoni Aubameyang

Muktasari:

  • Mshambuliaji huyo amefukuzwa kwa kosa la kwenda klabu ya usiku na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Ousmane Dembele.

 Kinara wa mabao wa klabu ya Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang ametimuliwa.

Mshambuliaji huyo amefukuzwa kwa kosa la kwenda klabu ya usiku na mchezaji wa zamani wa timu hiyo Ousmane Dembele.

Nahodha huyo wa timu ya taifa ya Gabon, alikosa mchezo wa Ligi Kuu Ujerumani dhidi ya Stuttgart uliochezwa jana kwa utovu wa nidhamu.

Dortmund imetoa taarifa ya mpachika mabao huyo kutimuliwa imetokana na tabia ya utovu wa nidhamu.

Nyota huyo alikwenda katika klabu ya Barcelona akiwa ameongozana na kaka yake Willy kabla ya kupiga picha na kuiweka katika mtandao akionekana yuko kwenye starehe.

Mchezaji huyo alitumia siku mbili kuponda raha mjini Barcelona baada ya kutoka katika mechi ya timu ya taifa.

Hii ni mara ya pili Aubameyang anaingia matatani, awali aliondolewa katika kikosi kilichokuwa kikijiandaa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kuhudhuria shereha ya kuzaliwa kwa rafiki yake mjini Milan.