Salamba nina deni kubwa Simba
Muktasari:
Salamba anawania namba pamoja na Bocco, Mohamed Rashid 'Mo Rashid', Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Marcel Kaheza na Shiza Kichuya.
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Adam Salamba amesema ushindani ndani ya kikosi hicho ni mkubwa hivyo ili mambo yaende sawa lazima kazi kubwa ifanyike.
Salamba aliyesajiliwa msimu huu akitokea Lipuli FC ya Iringa, ameanza kuichezea timu hiyo kwa dakika tano na aliingia kuchukua nafasi ya John Bocco 'Adebayor' katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Alisema: "Ushindani ni mkubwa ndani ya kikosi chetu hivyo kazi kubwa lazima ifanyike. Simba ina wachezaji wengi wenye uwezo hivyo natambua jukumu langu kubwa ni kupambana ili nikae kwenye nafasi nzuri ndani ya timu."
Alisema anatambua wadau wa soka na mashabiki wa Simba kwa ujumla wanamwamini hivyo atahakikisha anafanya kazi nzuri ndani ya kikosi hicho: "Kikubwa ni kufanya kazi tu na wasichoke kunipa ushirikiano."
Salamba anawania namba pamoja na Bocco, Mohamed Rashid 'Mo Rashid', Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Marcel Kaheza na Shiza Kichuya.
Hata hivyo, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefafanua namba anavyowatumia washambuliaji hao kwa kuwapa nafasi kila mmoja ili kulingana na namna wanavyoelewana kimchezo ili kupata matokeo mazuri.
"Naimani uwezo wa kila mchezaji na ndiyo maana namna nafasi kila mmoja ili kujua ni kwa namna gani wataisaidia timu,"alisema Aussems.