Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Omog, Nsajigwa ushindi lazima

Dar es Salaam. Makocha wa Yanga na Simba kila mmoja ameonyesha matumaini ya ushindi katika mchezo wa leo utakaoanza muda mfupi ujao.

Kocha mkuu wa Simba, Joseph Omog amesema watajitahidi kushinda mchezo huo ili kurejea kileleni mwa msimamo wa ligi, lakini amekiri itakuwa mechi ngumu kwani wapinzani wao ni timu nzuri.

"Tumefanya maandalizi mazuri ili kushinda mchezo huo.Tutajitahidi kutafuta matokeo kwani najua  hii ni mechi kubwa na ngumu"alisema Omog

Malengo yetu ni kushinda na kureja kileleni kwani hii ni ligi kila anayejitahidi ana nafasi kubwa ya kuongoza ligi.Ngoja tuone itakavyokuwa lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda mchezo huo.

Naye kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa'Fuso' alisema wamewaandaa wachezaji wao kimazoezi na kisaikolojia ili kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo huo.

"Tuko kamili na tuko tayari kwani licha ya kukabiliwa na changamoto ya majeruhi lakini  wachezaji wengine waliopo wako fiti kwa ajili ya kuhakikisha timu inapata ushindi"

"Najua itakuwa mechi ngumu kwani tunakutana wapinzani wa jadi lakini  hatuna wasiwasi na hilo kwani tumefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo huo," alisema Nsajigwa.

Yanga (4-3-3): Youthe Rostand, Juma Abdul (C), Gadiel Michael, Andrew Vincent, Kelvin Yondani, Papy Tshishimbi, Raphael Daud, Pius Buswita, Ibrahim Ajib, Obrey Chirwa, Geofrey Mwashiuya.

Simba (4-4-2): Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohamed Hussein, Juuko Murushid, Method Mwanjali, James Kotei, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo, Haruna Niyonzima