Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nyota wa mchezo kuondoka na dau nono

Dar es Salaam. Mechi ya Simba na Yanga siku zote inautamu wake hiyo ni baada ya wadhamini wa wenza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), wanatarajia kumzawadia Sh 500,000 mchezaji atakayeibuka nyota wa mchezo”Man of the match” Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 15 sawa na Yanga, lakini Wekundu wa Msimbazi hao wamewazidi wenzao kwa idadi ya mabao ya kufunga, wakiwa wamecheka na nyavu mara 19, wakati watani wao wakiwa na 10.

Meneja Masoko wa Benki ya KCB Tanzania, Edgar Masato, alisema  wameamua kufanya hivyo ili kuwachochea wachezaji wa timu hiyo kuonyesha kandanda la kuvutia siku hiyo.

“Tukiwa kama wadhamini wenza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, tunajiona tunajukumu la kutoa hamasa kwa wachezaji na timu kwa ujumla kuonyesha kandanda la kuvutia ili kutoa burudani inayostahili kwa mashabiki wa soka nchini na kwingineko wanakofuatilia mchezo huo wa watani wa jadi,” alisema, Masato

Alisema kuwa wanaamini, kila mchezaji atajituma kadri ya uwezo wake wote ili kuonyesha kipaji chake alichojaaliwa na Mwenyezi Mungu na mwisho wa siku kuisaidia timu yake kupata ushindi na tunaamini taratibu zote zitakazofanywa na kamati ya Tuzo ya VPL iliyopo chini ya shirikisho la mpira wa miguu nchini kwa kumpata mchezaji nyota wa mechi hiyo.

Aliwataka wachezaji wa Yanga na Simba kuwatendea haki mashabiki wa soka kwa kuonyesha kandanda la kistaarabu ambalo ndilo hasa linalowafanya mashabiki kuacha shughuli zao na kumiminika uwanjani siku hiyo.

Aliongeza: “Tunaamini kwa kufanya hivyo, tutakuwa si tu tunautendea haki udhamini wetu, lakini pia kuchangia kutoa burudani kwa mashabiki wa soka, wakiwamo wateja wetu wa KCB.”

KCB imejitosa kudhamini ligi hiyo msimu huu ikiwa ni mara ya kwanza kufanya hivyo.