Mwanamke mwenye bahati Atletico, Real

Muktasari:

  • Hii ni mara ya kwanza baada ya miaka 88 watoto wa mama moja wagawana Atletico, Real

Nishangilia timu ipi? Hilo ndiyo swali atalokuwa nalo Py Laurence ni mama wa nyota wa Atletico Madrid, Lucas Hernandez na beki wa Real Madrid, Theo Hernandez wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa watani wa jadi wa Madrid kwenye Uwanja wa Wanda.

Hii ni mara ya kwanza kwa wawili hao kukutana uso kwa uso pia itakuwa ni mara ya pili kwa mechi hiyo kushudia watu wa familia moja kucheza mechi hiyo ilikuwa ni ndugu Olaso mwaka 1929.

Mama Laurence ameweka wazi ni jinsi ilivyokuwa vigumu kwake kuwaona watoto wake wacheza mechi hiyo ya Atletico dhidi ya Real Madrid.

"Siwezi kuwa na upande wa moja wao, nitakaa kuangalia wanavyocheza," alisema mama huyo.

"Kabla ya mchezo nitawaambia wasichezeane vibaya.

"Wanatakiwa wapambane, lakini wanatakiwa wajue wao ni ndugu.

"Najivunia kuwaona wanacheza soka, sina la ziada ninalotaka."