Mbao yataka wawili Yanga
Muktasari:
- Timu hiyo ya Mwanza inasera ya kusajili wachezaji chipukizi inaowatumia katika Ligi Kuu
Klabu ya Mbao inasaka saini za chipukizi wa Yanga, Edward Makka na Yusufu Mhilu kujiunga na timu hiyo.
Taarifa zinasema kuwa Mbao iliomba Yanga kuwapa wachezaji hao kwa mkopo, maombi ambayo bado hayajajibiwa na uongozi wa Yanga.
Katibu Mkuu wa Mbao, Daniel Naila licha ya kutokubali moja kwa moja kama waliomba wachezaji hao, amesema kwa sasa wanaangalia mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Majimaji utakaopigwa kesho Jumamosi mjini Songea.
Ameongeza kuwa kama Kocha atakuwa amewaona na kuvutiwa nao, ataongea naye kama anawahitaji kisha baada ya mchezo atatoa taarifa rasmi.
"Huenda alishawaona na kuvutiwa nao, ila kwa sasa tunapambana na mchezo wa Jumamosi na Majimaji, kwahiyo tukimaliza nitaongea naye kocha na sisi kama uongozi tupo tayari kutekeleza" alisema Naila.