Yanga kushusha vifaa kwa majaribio

Thursday December 7 2017

 

Taarifa za ndani zilizopo kuna uwezekano Yanga ikashusha mastraika mawili wapya na mmoja wao atachukua nafasi ya Donald Ngoma kama atashindwa kujinasua kwenye mtego aliopewa na mabosi wake wa Jangwani.
Mastraika hao wanakuja kujaribiwa kwa ya siku chache kabla dirisha dogo halijafungwa na iwapo wataliridhisha benchi la ufundi lililo chini ya Kocha George Lwandamina ambaye jana alianza kuwanoa vijana wake uwanja wa Uhuru litawapa mkataba wa kuitumikia timu hiyo.
Washambuliaji hao ambao MCL Digital ilikutajia mapema ni Badara Kella na Bensua Da Silva ambao tayari Yanga imeshafanya mipango ya kuwaleta nchini kwa lengo la kuangaliwa na kocha Lwandamina.
Wakala wa Bensua Adou Jean Martin amethibitisha kuwa Silva ambaye ni raia wa Guinea atakuwa nchini wakati wowote kuanzia kesho Ijumaa tayari kwa majaribio ya wiki moja.