Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Martin atuliza mashabiki wa Yanga

Muktasari:

Martin amekiri anatambua mashabiki wa Yanga, wana maumivu ya kufungwa na watani wao wa jadi Simba, hivyo ili kuwapunguzia adhabu hiyo ni kutumia fursa ya mashindano ya kimataifa.

Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Martin amesema anaamini furaha ya mashabiki wao kwa msimu huu ni wao kufanya vizuri katika Kombe la Shirikisho Afrika.

Martin amekiri anatambua mashabiki wa Yanga, wana maumivu ya kufungwa na watani wao wa jadi Simba, hivyo ili kuwapunguzia adhabu hiyo ni kutumia fursa ya mashindano ya kimataifa.

"Mechi ya watani inaumiza kutokana na utani unakuwepo baada ya mechi kumalizika, hatukupenda matokeo yawe hivi ila hatuna budi kupambana na kuangalia ya mbele.

"Naamini tukifanya vizuri kimataifa, itafuta kila kitu kwani tutakuwa tumeweka historia ya aina yake ambayo haitafutika vizazi na vizazi vitakavyokuja nyuma yetu," alisema Martin.