Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Lwandamina asaini dili jipya

Muktasari:

Lwandamina amemalizana na Yanga ikiwa ni siku chache baada ya kuikomalia Simba katika pambano la Ngao ya Jamii kabla ya mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penalti ambapo Simba walishinda mikwaju 5-4.

GEORGE Lwandamina amethibitisha kukubaliana na Yanga na kwamba ataendelea kuinoa timu hiyo msimu huu hivyo mashabiki washushe pumzi.

Lwandamina amemalizana na Yanga ikiwa ni siku chache baada ya kuikomalia Simba katika pambano la Ngao ya Jamii kabla ya mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penalti ambapo Simba walishinda mikwaju 5-4.

Licha ya kipigo hicho, viongozi wa Yanga wameridhishwa na uwezo wa kikosi chao hatua iliyorahisisha maamuzi hayo ya kubakizwa kwa Lwandamina.

Mabosi wa Yanga walitarajia kumsainisha kocha huyo mkataba wa miaka miwili jana Ijumaa jioni na inadaiwa kwenye kikao cha ndani amewaambia kwamba sasa ndio Yanga itaanza kucheza mpira wake.

Ukiachana na mambo ya masilahi ya fedha yaliyoboreshwa zaidi ambayo hayakuwekwa wazi, pia wamempa kocha huyo gari ya kisasa baada ya kuona awali hakuwa na gari imara aliyokuwa akiitumia tangu atue Yanga.

Mbali na gari, pia wamemkodishia nyumba maeneo ya Masaki ambako kunasikika milio ya maji na mvumo wa upepo wa bahari tu.

“Nafurahi kusema nimemalizana na vongozi wa Yanga, ni heshima kubwa, siku zote nimekuwa nikisema hii ni klabu kubwa ina uzito wake,” alisema Lwandamina ambaye juzi ilizushwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anaondoka Yanga.

Pia katika kikao cha viongozi hao kuliwasilishwa ujumbe wa mwanachama maarufu, Yusuf Manji.

“Tulipomwambia tumefungwa na Simba alituambia amesikia, lakini amefurahi kusikia Yanga ilicheza soka zuri na kuwaomba wanachama wamwombee matatizo yake yaishe arudi na kushirikiana nasi,” alisema bosi mmoja wa Yanga.