Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba wamgomea Liuzio

Muktasari:

Liuzio aliyekuwa na kutambulishwa kwenye ulimwengu wa soka na klabu ya Mtibwa Sugar  ambayo Liuzio aliyekuwa na kutambulishwa kwenye ulimwengu wa soka na klabu ya Mtibwa Sugar  ambayo

baadaye ilimuuza kwenda  Zesco ya Zambia. Akiwa huko alicheza takribani misimu miwili na watatu aliondoka akajiunga na Simba..

HARAKATI za klabu ya Singida United  ya Mholanzi Hans Pluijm kumnasa straika wa Simba, Juma Liuzio, ni kama zimegonga mwamba kwa sababu Wekundu hao wa Msimbazi hawataki kumuachia.

Singida inamuhitaji Liuzio kwa ajili ya kuongezea nguvu kikosi chake kwenye mzunguko wa pili baada ya kurizishwa na kiwango chake.

Rafiki wa karibu wa Liuzio amesema, ni kweli Singida wanamuhitaji mchezaji huyo lakini Simba imeonyesha dalili zote kuwa haitaki kumuachia.

"Kweli Singida inamtaka,  Liuzio lakini Simba wamegoma, hawataki kumtoa sasa sijui kwa nini wakati

wenyewe hawampi nafasi kubwa ya kucheza. Bora wangemtoa akajaribu maisha mengine huko,"alisema.

Liuzio mchezaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, klabu  iliyomlea na kumuuza Zesco ya Zambia, alirudi nchini mwaka jana akasajiliwa kwa mkopo na Simba anayoichezea mpaka sasa.