Kibadeni ataka Matola apigwe za kutosha
Muktasari:
wawili hao kwa nyakati tofauti wamewahi kuwa wachezaji na baadaye makocha wa Simba
Dar es Salaam. Kocha wa zamani wa Simba, Abdallah Kibaden amewaambia wachezaji wa timu hiyo, kuhakikisha wanafunga mabao mengi mchezo dhidi ya Lipuli, ili wazidi kuwaacha mbali wapinzani wao Yanga.
Lipuli ipo chini ya makocha Amri Said na Seleman Matola ambao ni wanachama hai na wachezaji wa zamani wa Simba keshokutwa Jumapili watakuwa kwenye Uwanja wa Uhuru kuwavaa vinara wa ligi hiyo Simba.
Kitendo cha Yanga kuwafunga Mbeya City mabao 5-0, alisema kiwe ishara kwao kujua kasi ya wapinzani wao inavyoweza kuwavunja nguvu itakapofikia hatua ya kupishana pointi moja moja.
"Wasipunguze kasi ya mabao, kila mechi angalau wafunge bao tatu, zinaweza kuwasaidia kulingana na msimamo wa ligi ulivyo mgumu,hilo ndilo linalowafanya wawe juu ya Azam,"
" Ni kweli kila timu imejipanga kwa ushindani, lakini Simba ina wachezaji wazoefu ambao wanaweza kuamua mechi,hao wanatakiwa kujua majukumu yao bila ya kusukumwa sukumwa,"alisema
"Ustaa unakuwa hauna maana endapo timu inakuwa na matokeo yasiyoridhisha, lakini inapendeza zaidi timu inapofanikiwa ikiwa chini ya mastaa,hivyo wajue wajibu wao ndipo Simba inaweza kuwa na jipya msimu huu,"alisema.