Jalada la Aveva latupwa Takukuru

Muktasari:

  • Viongozi hao wa Simba wanakabiliwa na makosa ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha

 Jalada la kesi inayowakabili viongozi wa Simba akiwemo Rais wake, Evans Aveva na mwenzake lililokuwepo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) limerudishwa Takukuru.

Hayo yameelezwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mwambapa na Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai.

Swai alidai kuwa jalada hilo limerudishwa juzi Takukuru kutoka kwa DPP na ametoa maelezo ya kukamilisha zaidi upelelezi.

Hayo yameelezwa baada ya Wakili wa Utetezi, Philemon Mutakyawa kuuliza juu ya jalada hilo lililokuwepo kwa DPP limefikia wapi.

Aveva na makamu wa rais wa klabu hiyo, Godfrey Nyange ‘Kaburu’, wanakabiliwa na Mashtaka matano ya uhujumu uchumi.

 

 

Ikiwamo ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha wa Dola za Marekani (USD) 300,000.