Mbeya City yajiapiza kwa Mbao FC
Muktasari:
Akitoa sababu ya kauli yake ya kujiamini kwamba anaamini katika dhamira ya kufanya kitu cha kipekee anapokuwa ndani ya uwanja na kwamba ni rahisi kufanikiwa.
STRAIKA wa Mbeya City, Victor Hangaya amesema wameweka nia na dhamira kuhakikisha mchezo wao na Mbao FC, kesho kutwa Ijumaa wanapata matokeo.
Akitoa sababu ya kauli yake ya kujiamini kwamba anaamini katika dhamira ya kufanya kitu cha kipekee anapokuwa ndani ya uwanja na kwamba ni rahisi kufanikiwa.
"Ligi hii si ya kulala hata dakika moja, ushindani ni wa juu kila timu inataka kuweka misingi imara mapema na siyo kuanza kuumiza kichwa wakati ligi ikielekea mwisho,"
"Najua Mbao FC, ina nyota wanaojua kupambana, hilo halituumizi badala yake ni kuongeza umakini wa kazi ili tuweze kufanikisha lengo letu," anasema.