AFC Leopard, Simba zakamiana kinoma
Dar es Salaam. Nahonda wa AFC Leopard, Azizi Okaka amesema wanaiheshimu Simba kutokana na ukubwa wao lakini wamesafiri kwa lengo la kushindana na siyo kukubali kushindwa.
Simba na Leopard wanatarajia kushuka uwanjani kesho saa 12 jioni kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam ukiwa ni mchezo wa kirafiki.
Nahodha Okaka alisema kikosi chao kimejiandaa vizuri tayari kwaajili ya mchezo huo ambao wanatarajia kuutumia kukiandaa kikosi ikiwa ni pamoja kutengeneza vijana waweze kufiti katika mfumo wa mwalimu.
"Kwa asilimia kubwa wachezaji wengi waliopo katika kikosi chetu ni chini ya miaka20 mwalimu anatarajia kutumia mchezo huo kuwapa uzoefu wa kucheza mechi kubwa," alisema Okaka.
"Tunaamini mchezo utakuwa mzuri na utatusaidia kutuweka fiti zaidi baada ya kufanya mazoezi kwa muda mrefu bila kucheza mchezo wa kirafiki," alisema.
Wakati huo huo nahodha msaidizi wa Simba, Deogratus Munish 'Dida' alisema wachezaji wote wa wapo fiti tayari kwa mchezo huo.
Alisema wamejiandaa vizuri na kila mchezaji yupo katika hali ya mchezo wanategemea mchezo mzuri na wa ushindani kesho, alitumia nafasi hiyo kuwaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuwapa ushirikiano.