Nduda kiroho safi, aanza upya Simba

Muktasari:

  • Nduda aliyesimamishwa katika kikosi hicho hali na hakutambulishwa katika Tamasha la Simba Day amerejeshwa kikosini baada ya pande zote mbili kukaa chini na kuelewana.

Dar es Salaam. Kipa Said Mohammed ‘Nduda’ ameanza upya katika kikosi cha Simba, baada ya kuonekana kubadili kabisa staili ya nywele zake kwa kutoa kiduku kichwani na kuwa umakini kila zoezi lililokuwa linatolewa na kocha wake wa makipa Mohammed Mwalami.

Nduda aliyesimamishwa katika kikosi hicho hali na hakutambulishwa katika Tamasha la Simba Day amerejeshwa kikosini baada ya pande zote mbili kukaa chini na kuelewana.

Nduda alisema baada ya kukaa nje kwa muda mrefu amejifunza vitu vingi vya nje na ndani ya mpira, hivyo kurejea kwake katika kikosi anataka kuwa bora zaidi.

“Hahahaha nimeamua kuzipunguza tu, kweli nilikuwa nje lakini nilikuwa najifua kama kawaida na nimerudi kazini kikubwa kilichobaki ni kuipambania timu yangu ilifanya vizuri.”

Akizungumzia changamoto ya namba kutokana na makipa waliopo, Aish Manula, Ally Salum na Deogratius Munishi kuonekana kuingia katika mifumo ya kocha Mbelgiji, Patrick Aussems, alisema suala hilo anamuachia mwalimu katika kupanga, lakini kikubwa wote ni wachezaji wazuri kikubwa matokeo yapatikane mazuri.