Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtogo wa Dicha saluti kwa Ninja

Muktasari:

  • Lwandamina alimwangalia kwa makini beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kisha akasema huyu ataziba pengo la Yondani na kuanza kumfua na juzi Jumamosi, Ninja akathibitisha si mtu wa kuchezea pale aliposhirikiana na Andrew Vincent ‘Dante’ kuweka ukuta wa maana. Hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa Ninja tangu asajiliwe kutoka Taifa Jang’ombe ya Zanzibar.

HABARI za Yanga kumkosa beki wake, Kelvin Yondani kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, zilishtua mashabiki wa mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara, lakini kocha George Lwandamina, akawashusha presha.

Lwandamina alimwangalia kwa makini beki Abdallah Shaibu ‘Ninja’ kisha akasema huyu ataziba pengo la Yondani na kuanza kumfua na juzi Jumamosi, Ninja akathibitisha si mtu wa kuchezea pale aliposhirikiana na Andrew Vincent ‘Dante’ kuweka ukuta wa maana. Hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza ya kimataifa kwa Ninja tangu asajiliwe kutoka Taifa Jang’ombe ya Zanzibar. Sasa yule straika matata wa Welaytta Dicha, Mtogo Arafat Djako amempigia saluti kwa kusema jamaa ni bonge la beki.

“Yanga wamecheza vizuri sana hasa sehemu ya beki na winga. Mchezaji ambaye alitupa wakati mgumu ni yule beki wa kati mrefu si yule mwenye rasta ni yule namba 6 nafikiri (Ninja). Alicheza vizuri na amechangia kuharibu mipango yetu,” alisema Djako.

Kwa upande wa beki wa kati wa Welaytta, Bzabih Melayu alisema: “Yanga ni wazuri hivyo tunakwenda kujifua ili kuhakikisha hatufanyi makosa, kwetu tutawafunga kwetu bila wasiwasi.”

Katika mchezo huo, Yanga walishinda mabao 2-0 na watacheza tena mechi ya maruadiano nchini Ethiopia Aprili 18.