Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Barker amtuliza kiungo Simba

SIMBA Pict


WAKATI klabu tatu kutoka Ulaya zikiripotiwa kuwania huduma ya kiungo mshambuliaji wa Simba, Anicet Oura ambaye alifanikiwa kuonyesha kiwango cha juu msimu uliomalizika 2025-2026, ni kama Wekundu hao wa Msimbazi wamemsikiliza kwa umakini kocha wa kikosi hicho, Steve Barker, kisha kufanya uamuzi mgumu wakisema: “Oura anabaki, haendi popote.”


Kiungo huyo raia wa Ivory Coast, alitua Simba kipindi cha usajili wa dirisha dogo la Januari 2026, ambapo hadi msimu wa 2025-2026 unamalizika, alicheza kwa kiwango kikubwa kilichozivutia klabu hizo ambazo ni Bursaspor ya Uturuki, Vi­kingur Reykjavik ya Iceland na DAC 1904 Dunajska Streda ya Slovakia.


Wakati kukiwa na taarifa hizo, Barker ameonyesha wazi kuwa Oura ni sehemu ya mipango yake kuelekea msimu ujao, akiamini bado ana uwezo mkubwa wa kuisaidia timu hiyo baada ya kuzoea soka la Tanzania.

OU 01

Hoja hiyo ya Barker, imemuibua kiongozi mmoja wa Simba aliyeliambia Mwanaspoti kwamba wanaelekea kushinda vita ya kumbakisha Oura ambaye Bursaspor ya Uturuki ndiyo iliyoonekana kumuhitaji zaidi ikielezwa imejipanga kuwasilisha ofa ya Euro 250,000 ambazo ni zaidi ya Sh 750 milioni.

Bosi mmoja wa juu wa Simba anayesimamia usajili ameliambia Mwanaspoti kuwa mpaka jana hakukuwa na ofa yoyote rasmi kuhusu Oura na kwamba bado wana mipango ya muda mrefu na raia huyo wa Ivory Coast.

“Hizo taarifa za Oura kuondoka hazina ukweli, mpaka sasa hakuna ofa ambayo imefika kwetu, tunasikia tu kwenye mitandao, anayemtaka mchezaji angekuja Simba, tuna hesabu kubwa na Oura kwahiyo bado yupo sana hapa Simba, haondoki,” amesema bosi huyo.

OU 02

Oura mwenye miaka 26, alijiunga na Simba akitokea IF Gnistan ya Finland kwa mkataba wa miaka miwili na tangu kutua Msimbazi amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika mafanikio ya timu hiyo msimu huu.

Kiungo huyo mshambuliaji ameisaidia Simba kutwaa mataji mawili ya Kombe la CRDB na Muungano huku akionyesha uwezo mkubwa katika eneo la kiungo mshambuliaji kwa kufunga mabao sita na kutoa asisti tatu kwenye ligi ambako Wekundu hao wa Msimbazi wamemaliza nafasi ya pili na pointi 73, nyuma ya Yanga iliyotwaa ubingwa kwa tofauti ya pointi mbili.

Uwezo wake wa kucheza nafasi tofauti kwenye safu ya ushambuliaji, kasi, nguvu na uwezo wa kutengeneza nafasi, umeifanya thamani yake kuanza kupanda kwenye soko la usajili.

OU 03

Kabla ya kujiunga na Simba, Oura amepitia klabu mbalimbali zikiwemo Gnistan ya Finland, Muaither SC ya Qatar, Stellenbosch FC ya Afrika Kusini na ASEC Mimosas ya Ivory Coast kote akitajwa kama mmoja kati ya wachezaji mahiri.

Bursaspor si ngeni kwa Oura, kwani klabu hiyo ilikuwa imeanza kumfuatilia tangu kipindi ambacho kiungo huyo alipokuwa akicheza soka la kulipwa Finland kabla ya kukumbwa na majeraha.

Awali ilielezwa kwamba, wakati Oura akiwa katika rada za kuondoka, Simba ndiyo maana ikaanza mchakato wa haraka kuwania saini ya winga wa Afrika Kusini, Keletso Makgalwa kutoka Sekhukhune ya nchini humo, huku dili hilo likikamilika kwa mkataba wa miaka miwili.

Kwa Simba kukamilisha usajili wa Makgalwa, maana yake ni kwamba, eneo la kiungo mshambuliaji msimu ujao litakuwa na nguvu zaidi kutokana na Msauzi huyo anakwenda kuungana na Elie Mpanzu, Libase Gueye na Oura waliofanya vizuri tangu ujio wa Kocha Barker.