Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Singida Black Stars kupindua dili la Mkenya

SINGIDA Pict

Muktasari:

  • Kagera Sugar iliyorejea Ligi Kuu Bara ikitarajiwa kushiriki msimu wa 2026-2027 baada ya kushuka msimu wa 2024-2025, ilikuwa katika hatua za mwisho za kuipata saini ya mshambuliaji huyo, japo juzi uongozi wa Singida ulikutana naye na kufanya mazungumzo chanya.

WAKATI uongozi wa Kagera Sugar ukiwa katika hatua za mwisho za kuipata saini ya mshambuliaji wa Pamba Jiji, Mkenya, Mathew Tegisi Momanyi, ghafla mabosi wa Singida Black Stars wameingilia kati dili hilo na sasa vita imeanza upya.

Kagera Sugar iliyorejea Ligi Kuu Bara ikitarajiwa kushiriki msimu wa 2026-2027 baada ya kushuka msimu wa 2024-2025, ilikuwa katika hatua za mwisho za kuipata saini ya mshambuliaji huyo, japo juzi uongozi wa Singida ulikutana naye na kufanya mazungumzo chanya.

SING 01

Chanzo kutoka kambi ya timu hiyo, kimeliambia Mwanaspoti mazungumzo hayo yameenda vizuri kwa ajili ya nyota huyo kujiunga na Singida msimu wa 2026-2027, huku Kagera Sugar ikipigwa bao baada ya mchezaji mwenyewe kuonyesha pia utayari huo.

“Bado hajasaini mkataba lakini mazungumzo yake na Singida yameenda vizuri na muda wowote huenda makubaliano hayo yakafikiwa kati ya pande zote mbili, ni mchezaji mzuri tunayeamini atakuwa chachu ya mafanikio,” kilisema chanzo hicho.

SING 02

Akizungumza na Mwanaspoti, Momanyi amesema kwa sasa ni mapema kuzungumzia sehemu atakayocheza msimu ujao, licha ya ofa mbalimbali zilizopo, japo uamuzi wa mwisho ataufanya baada ya kukaa chini na menejimenti yake na kuangalia timu sahihi.

Momanyi aliyetokea Shabana ya Kenya, alijiunga na Pamba dirisha dogo la Januari 2025 na hadi mwisho wa msimu wa 2024-2025, alifunga mabao saba ya Ligi Kuu, akiwa ndiye aliyeongoza katika kikosi hicho.

SING 03

Nyota huyo aliendeleza alipoishia akiwa na Shabana FC, kwa sababu kabla ya kujiunga na Pamba alikuwa pia amefunga mabao matano kwao Kenya, nyuma ya mshambuliaji mwingine wa kikosi hicho, Brian Michira aliyekuwa anaongoza kwa kufunga saba.

Mshambuliaji huyo akaendeleza tena kiwango bora akiwa na Pamba Jiji, baada ya kumaliza msimu wa 2025-2026 katika Ligi Kuu Bara akifunga mabao 11, akiwa ndiye nyota aliyeongoza pia ndani ya kikosi hicho, ikiwa ni msimu wake wa pili mfululizo.